TBC1 wapo kazini wanajua jamaa anataka kuchafua upinzani na ndio maana wanampa nafasi ili amtukane Slaa na wengine
yeye anagombea ubunge wa jimbo la kawe kwa nini apewe airtime ya kuonekana Tanzania nzima, kwani anagombea uraisi?
Hivi jamani hii nafasi ya vyama kupewa Airtime na TBC ni kwa ajili ya Urais au na ubunge?
Sioni kama kuna tija kufanya kampeni ya Ubunge wa jimbo moja kwa matangazo ya Nchi nzima wakati mgombea Urais wa chama hicho hicho hajawahi kusikika zaidi ile show ya ATN.
Mbatia kwa hapo sijakuelewa.
Huyu Mzee Hashim amekuwa kama ndio Mgombea ubunge halafu Mbatia mgombea urais, maana hata kampeni za mikoani tumewahi kusikia huko Kigoma aligombea gari na Mgombea ubunge na mgombea wao baada ya kujikuta mgombea urais hana usafiri.
Ahh kwa pembeni kuna DJ anapiga jingle la Mbatia!
Heshima kwako Kituko,
Kwani kuna tatizo gani Mbatia akipewa airtime TBC1.Unajua wakati mwingine napata taabu kidogo kuwaelewa wanajamvi wanataka nini haswa.Ingekuwa mgombea ni CCM ningewaunga mkono Mbatia anajua mgombea urais hana nafasi lakini ana haki ya kupewa airtime na TBC 1 kama ilivyo kwa wagombea wengine wa nafasi ya urais Dr Slaa wa CHADEMA na Lipumba wa CUF washapewa nafasi hiyo hadhimu.NCCR Mageuzi wameelekeza nguvu kwa mwenyekiti wake shida iko wapi ? .