Kampeni ya "Nakupenda Wanipenda,na TUPEANE MIKONO".

Kampeni ya "Nakupenda Wanipenda,na TUPEANE MIKONO".

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
TUPEANE MIKONO.


1.Tukipeana mikono,ni ishara ya upendo
Kuna ua migongano,mikono funzo la jando
Waonao mgangano,hao wana mbovu nyendo
Nakupenda wanipenda,tupeane na mikono.


2.Tukipeana mikono,hilo jambo la imani
Ila aso na maono hawezi ona rohoni
Wahofiya konokono,wakti yupo mkononi
Nakupenda wanipenda,na tupeane mikono.


3.Kama magonjwa ni hoja,tunayo kubwa hatari
Tulopaswa ni kungoja,siyo kuanza habari
Mwisho vizuke viroja,tuitwe wenye viburi
Nakupenda wanipenda, na tupeane mikono.


4.Mpishi anapopika,hatumii maroboti
Kinyaa ungetapika,wonapo pishi chapati
Kwa mikono zakandika,mkate na kalimati
Nakupenda wanipenda,na tupeane mikono.


5.Hata pesa ukishika,mikono mingi tambua
Huko ilishapitika,kwako ikakufikia
Zianze chemshika,pesa sije angamia
Nakupenda wanipenda,na tupeane mikono.


6.Labda pia tungesema,magonjwa mapya yazuka
Yatupayo ukilema,mikono tukijishika
Ila tujue mapema,upendo tunauzika
Nakupenda wanipenda,na tupeane mikono.


7.Ukiona kwanza jua,we siyo muadilifu
Mikono hujasugua,kuosha wako uchafu
Ndo mana watusumbua,na kuleta usumbufu
Nakupenda wanipenda,na tupeane mikono.


8.Hapa ungelianzia,jamii kuelimisha
Usafi kuzingatia,macho singe tupofusha
Mbali tungejionea,mikono tungesafisha
Nakupenda wanipenda,na tupeane mikono.


9.Leo tunaogopana,yamekua maajabu
Mikono si kupeana,twaanza unda sababu
Magonjwa kuenezana,siyo njia ya kutibu
Nakupenda wanipenda, na tupeane mikono.


10.Mikono tutapeana,siku zote na daima
Hatutaweza nyimana,sisi ni watu si kima
Kiganja siyo kiatu,tuhofu kwamba kiama
Nakupenda wanipenda,na tupeana mikono.


SHAIRI-TUPEANE MIKONO.
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom