DOKEZO Kampeni ya 'Ng’arisha Katavi Tunza Mazingira' iliyoanzia katika Bwawa la Milala, imeishia wapi?

DOKEZO Kampeni ya 'Ng’arisha Katavi Tunza Mazingira' iliyoanzia katika Bwawa la Milala, imeishia wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mliogwa

Member
Joined
Jun 6, 2024
Posts
37
Reaction score
37
Wakati napita katika eneo la Bwawa la Milala, Manispaa ya Mpanda unapojengwa mradi mkubwa wa maji wa Miji 28, nilikumbuka kampeni kubwa ya Ng’arisha Katavi Tunza Mazingira iliyolenga kupanda miti Milioni 10.

Kampeni hiyo iliyozinduliwa 24/01/2023 hadi 26/10/2023 na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko kwa lengo kuhamasisha utunzaji wa mazingira, lakini nilichobaini ni kuwa kwa sasa hakuna mafanikio katika eneo waliloanza kufanya uzinduzi.

Moja ya eneo la Bwawa la Milala ilipopandwa miti mingi, hiyo miti haipo tena ni kama vile haikupandwa na imebakia miti ya zamani ambayo muonekanao wake ni kama vichaka.

Naimani kampeni hiyo ilitumia gharama fulani ya fedha, ni aibu miti hiyo kuachwa na kujifia, ninaomba wenye mamlaka kuhuwisha Kampeni hiyo kwa sababu uhifadhi wa mazingira una raha yake na ni faida kwa wengi.
photo_2024-12-04_16-28-02.jpg

Mkuu wa Mkoa alipokuwa akipanda mti katika eneo la bwawa la Milala Manispaa ya Mpanda, Januari 2023.
photo_2024-12-04_16-28-14.jpg

photo_2024-12-04_16-28-22.jpg

photo_2024-12-04_16-28-33.jpg

Pia soma ~ Serikali yapanda miti mingine zaidi ya 400 eneo la Milala (Mpanda - Katavi) baada ile ya awali kunyauka
 
Back
Top Bottom