Kampeni ya Tezi Dume

Kampeni ya Tezi Dume

MicJay

Member
Joined
Apr 19, 2014
Posts
75
Reaction score
29
Baada ya Rais wetu kwenda ng'ambo kuchekiwa afya na kukutwa na tatizo la Tezi dume na akafanyiwa upasuaji.

Taarifa ya habar jana,ambayo ilitolewa na waziri asie na wizara maalum kwamba mwanzoni mwa mwaka 2015 kutakuwa na kampeni za kupima Tezi Dume kwa wanaume wote na watakaokutwa na tatizo watatibiwa hapahapa nchini na Hiyo kampeni itazinduliwa na wazir huyo asie na wizara maalum.

Kampeni hii wanasema itawahusu zaidi wanaume wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea.Wanaume wenzangu mi nafikiri kabla ya kampeni hizo tungejiuliza ugonjwa huo unasababishwa na nini, tukijua kisababishi ndo tunawezajua kwamba kunauwezekano wananchi wa kawaida wakawa nao.

Ila tofauti na hapo, unaweza ukaambiwa una Tezi Dume wakufanyie upasuaji baada ya hapo we kuzaa ikawa basi tena.Tujiulize kwanza ndugu zetu!
 
Tanzania tena Hospitali ya Taifa Ashapasuliwa mtu kichwa badala ya goti.

Na hiyo story kwa nini ailete waziri asiye na wizara maalum? Ambao wengi tunajua ndio bos wa TISs / inteligensia kwa wapinzani badala ya Waziri mwenye wizara husika?
 
Baada ya Rais wetu kwenda ng'ambo kuchekiwa afya na kukutwa na tatizo la Tezi dume na akafanyiwa upasuaji.Taarifa ya habar jana,ambayo ilitolewa na waziri asie na wizara maalum kwamba mwanzoni mwa mwaka 2015 kutakuwa na kampeni za kupima Tezi Dume kwa wanaume wote na watakaokutwa na tatizo watatibiwa hapahapa nchini na Hiyo kampeni itazinduliwa na wazir huyo asie na wizara maalum.
Kampeni hii wanasema itawahusu zaidi wanaume wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea.Wanaume wenzangu mi nafikiri kabla ya kampeni hizo tungejiuliza ugonjwa huo unasababishwa na nini,tukijua kisababishi ndo tunawezajua kwamba kunauwezekano wananchi wa kawaida wakawa nao.Ila tofauti na hapo,unaweza ukaambiwa una Tezi Dume wakufanyie upasuaji baada ya hapo we kuzaa ikawa basi tena.Tujiulize kwanza ndugu zetu!
Mkuu MicJay Mbona hilo suala tumeshalizungumzia sana hapa jukwaani. Hebu tembelea bonyeza hapa.[h=1]Topic: Kuvimba kwa Tezi Dume (Benign Prostate Hyperplasia BPH) Featured[/h]
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Micjay, unataka kutuambia kuwa huyo Waziri wako asiye na Busara, sorry Wizara, Maalumu hajui kuwa Mwakani kuna Kampeni za Uchaguzi Mkuu? Tutakuwaje na Kampeni mbili kwa wakati mmoja?
 
Bado sijajua tezidume ni nini kwa uhakika. Hata hivyo kama watu watahamasika na kwenda kupima nashauri wasikubali operation kwani zinaweza kuondolewa zile nzima.

Waende huko huko John Hopkins au St Thomas
 
Tezi Dume kwa kuwa Rais ameugua... kesho akiugua gonjwa lingine wataendesha kampeni ya gonjwa hilo?!

Serikali makini haiwezi kuendesha kampeni dhidi ya tatizo moja la afya... inaimarisha huduma za afya za msingi na kila kitu kitanyooka. Wahache kuongopea Watanzania!!
 
Nimeisoma hiyo thread na nimeielewa,nashukuru Mzz mkavu.Ila hofu yangu inakuja kwass wabongo ikigundulika wengi tuna hilo tatizo.

PpUnadhani tutafanyiwa matibabu kwa nia njema? Au ndo tutafungwa vizazi?
 
Back
Top Bottom