Ngosha ze Dong
Member
- Feb 18, 2015
- 20
- 4
"Fahari ya kijana ipo katika nguvu zake na uzuri wa mzee ni kichwa chenye mvi (Mithali 20:29)."
Tambua kuwa ujana huishi katika maono na uzee katika kumbukumbu. Yote haya yako chini ya WAKATI.
THAMANI YA WAKATI.
WAKATI;
Wakati uliumbwa kwenda mbele daima na si kumsubiri mtu. Na ukipita, haupatikani tena; na haupo wakati unaotosha. Hata uonekanao wa kutosha, hutokea kuwa hautoshi kwa kawaida. Wakati Uliopita unaumiza zaidi kuliko Ujao, na Ujao unatia hofu kuliko tulionao, kwani tulionao hautoshi. Usiupoteze kwa kuishi maisha ya mwingine, bali utumie katika kutimiza malengo yako.
Wakati ni fursa kwa kijana akiutumia katika mambo makuu yafuatayo.
1. FURSA;
Fursa ni kitengo muhimu sana Katika Maisha ya Mwanadamu kwani ndio chanzo Cha kusonga mbele kwake. Fursa inalewa na mambo mawili; KAZI na KUWAJIBIKA.
A. KAZI,
Huwezi kupendeza Kama hufanyi kazi. Kazi ndio nyota pekee ya maisha ya mtu. Ujana unaanzia katika kufanya kazi, na ndio Wakati sawia wa kufanya kazi kwani uzeeni hakuna nguvu za kupambana na maisha. Ujana si kujenga majungu bali Kutengeneza mkate wa kutumia. Katika Maisha, kijana anasifiwa kwa kukosolewa na si kwa kusifiwa. Kwa sababu sifa zinaua; na ukiona hukosolewi jua kuna tatizo sehemu. Kukosolewa ni ishara ya uwezo wako wa kufanya jambo la maana na lililobora kwa baadae. Mafanikio yoyote hayaji bila Matusi. Ukisoma Biblia kitabu Cha Mwanzo 2:15.
Kinazungumia kuilinda bustani ya Edeni kwa kuitunza, maana yake kufanya kazi. Sifa pekee ya kijana ni kuchakarika. Uzuri na Utanashati hauchemshwi chakula.
Haitatokea siku chakula kimeisha ukachemshwa uzuri wa mtu, La hasha! Uzuri ni matangazo ya utu wa mtu na si utu kamili. Huwezi kupendeza Kama hufanyi kazi. Kazi ndio Nyota pekee ya Maisha. Bahati mbaya, Ujia wa Mafanikio ya mtu uko kwa Adui zake. Akiogopa kuupita, ataambulia majuto kutoka kwa marafiki zake. Na vijana wengi wanaogopa kupitia changamoto. Fahari ya kijana ni nguvu zake.
B. UWAJIBIKAJI:
Kuwajibika ni sehemu ya kazi ambako kunampa kijana faida mbili nazo ni (a)Kupata kanuni ya Kuishi na (b)Kanuni ya Kupata mtaji.
Nikianza na kanuni ya Kuishi, Katika kuwajibika kunampa mtu mali ya kujikimu Maishani. Tatizo kubwa vijana linawakumba ni kujikita katika tamaa na kuwa vigeugeu. Vijana wengi hawana msimamo.Tamaa ni kabuli la mafanikio ya mtu na kigeugeu ni jeneza la ndoto zake. Njia pekee ya kuyatoroka majanga haya ni kuwajibika.
Kanuni nyingine ni ya Kupata mtaji, kijana anapowajibika anatimiza malengo ya kiada kadri anavyoongeza kipato chake kutokana na juhudi zake. Kuutumia Wakati vizuri Katika kuwajibika ni kufungua njia ya baraka za Maisha ya mtu kwani kupitia kazi mtu anapata Fursa mbalimbali. Kuwa na matumaini makubwa kuliko juhudi za malengo ya mtu, ni kujinyima fursa mbele ya bahati yake. Bahati ni Juhudi, na sio Maneno. Ujana sio ngonjera ni kuwajibika.
2. AFYA:
Afya ni mtaji mkuu wa maisha ya mtu. Wakati unaanzia kwenye afya ya mtu hata yajayo hutengenezwa na afya ya leo. Kuutumia vyema ujana ni kutunza mwili kwa wakati uliopo. Afya inajengwa kuanzia mtu anapozaliwa ndio maana hunyonyeshwa. Na ujana ndio sehemu kubwa ya utunzaji mwili kwani unakuwa bado unanguvu ya kusharabu viini lishe vyote, na hivyo kupelekea afya bora uzeeni. Afya ni chanzo cha mambo mawili muhimu katika mwili wa Mwanadamu. Nayo ni Ubora wa Fikra chanya na Taswira chanya ya mtu. Ubora wa Fikra chanya unapelekea mtu kuwa kiongozi bora wa mawazo na busara. Na uongozi bora ni uwezo wa kutatua matatizo mbalimbali katika Jamii. Changamoto zikitatuliwa malengo yanakuwa yamefikiwa. Fikra chanya ndiyo toroli la Malengo ya mtu, mosi.
Pili, Taswira chanya inamfanya mtu ajikubali. Picha ya mtu ni imani yake. Anapojikubali anatengeneza kitambulisho Cha kujiamini. Kujiamini ni vita mbele ya Woga. Na hofu ni vita mbaya sana Katika Fursa na Maisha ya mtu. Katika Maisha, kuamini Vita mbele ya woga utafanikiwa zaidi kuliko kutukuza amani mbele ya unafiki. Woga unaua soko la ajira kwa vijana kwani unavunja majaribio.
Hivyo, kuepuka haya yote, ni ujana kuuandaa uzee, na siyo uzee kuujutia ujana.
3. ELIMU:
Elimu ndio kitengo maalum Cha afya na malengo ya mwanadamu kutimia. Ujana uliotukuka ni pamoja na kujikita katika kutafuta, kujifunza na kufunza elimu kwa Jamii nzima. Mataifa yanapanda juu au kuangamia kutokana na kundi kubwa la vijana kufanikiwa ama kuporomoka kiafya, kimaadili na kimtazamo. Taifa kuendelea ni matokeo ya kundi la vijana kuendelea. Na ili kijana aendelee lazima awekeze elimu na imani kwa kiwango kikubwa. Elimu inainua busara, ufahamu na elimu. Kulinganisha taarifa kwa ufasaha kunaleta tija katika matumizi ya busara. Ujana ni tunu kwa Taifa, elimu ikiwekezwa vizuri ndani yake.
Mwisho, kupitia kampeni ya Utumie Vyema Ujana ni dhahiri shahiri kuwa Kijana ataelimika juu ya matumizi bora ya wakati wake na mavuno sahihi ya umri wake uzeeni. Ujana ni jicho linaloangaza pande zote za changamoto na kuangalia wapi, kivipi na lini fursa zitatatulika ndani ya changamoto hizo. Kama thamani ya Mwili ni Jicho, na Jicho lenye Maono ndio Sura ya Utu, basi Ujana ni jicho la mwili.
Tuutumie Vyema Ujana kwani ndio tunu ya Taifa letu.
Karibuni sana kwa maoni, ushauri na maswali.
Mungu ni Mwema!

Upvote
1