Kampeni ya “Vote now” yazinduliwa TANAPA

Kampeni ya “Vote now” yazinduliwa TANAPA

PendoLyimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
969
Reaction score
1,055
KAMPENI YA “VOTE NOW” YAZINDULIWA TANAPA

Na Edmund Salaho/Arusha.

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limezindua kampeni mahususi ya kupigia kura vivutio vyake viwili ambavyo ni Hifadhi ya Taifa Serengeti na Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro ambavyo vinashindanishwa kama vivutio bora zaidi barani Afrika, Kampeni inayoenda kwa jina la VOTE NOW”

Akizungumza na vyombo vya Habari wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo “VOTE NOW”
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara July Beda Lyimo alisema,

“ Hifadhi ya Taifa Serengeti na Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro zimechaguliwa na Taasisi maarufu duniani ya World Travel Awards ikishindana na Hifadhi shindani kutoka Botswana, Namibia, Uganda, Afrika Kusini na Kenya, kwa upande wa Serengeti inashindana kama Hifadhi Bora Barani Afrika “Africa’s Leading National Park 2024” na kwa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro inashindana kama Kivutio Bora Afrika “Africa’s Leading Attraction 2024”.

Maeneo haya yamekuwa utambulisho wa Nchi ya Tanzania katika masuala ya Uhifadhi na Utalii kupitia Filamu ya "The Royal Tour" ambayo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alizitangaza Hifadhi za Taifa Serengeti na Kilimanjaro na kuiweka Nchi yetu katika Uso wa Dunia katika masuala ya Uhifadhi na Utalii ambapo kama Taifa tumeshuhudia matokeo chanya ya juhudi hizi za Mhe. Rais wetu.

“ Tumekuja kwa watanzania wote, wadau wa utalii kuwaomba tupige kura kwa wingi ili hifadhi hizi ziwe kidedea na kuaminika kutokana na sifa za kipekee zilizojaliwa. Ushindi huo utaongeza idadi ya watalii, mapato kwa taifa na kuongeza ajira kwa watanzania” aliongeza Kamishna Lyimo.

Aidha, Kamishna Lyimo alisema kuwa, kuzipigia kura hifadhi hizi kuna faida kubwa kwa Taifa letu na vivutio vyake kwani vitaendelea kufahamika zaidi duniani na wageni wataendelea kuja kuvitazama kwa wingi zaidi na tutaogeza idadi ya mapoto kama ambavyo ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyotuelekeza kufikia watalii million tano na mapato ya dolla billioni sita ifikapo mwaka 2025.

Hifadhi ya Taifa Serengeti imeshinda tuzo hiyo ya Hifadhi Bora Barani Afrika kwa mara tano mfululizo kuanzia mwaka 2019 hadi mwaka 2023 ambapo kwa kura yako mwaka huu 2024 itaiwezesha Hifadhi hii kushinda kwa mara ya sita mfululizo huku Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro imeshinda tuzo ya kivutio Bora Barani Afrika mwaka 2013, 2015, 2016, 2017, na 2018 ambapo kwa kura yako tutaleta ushindi huu nyumbani kwa mara ya sita. Ili kupiga kura zako tembelea tovuti ya www.worldtravelawards/vote.

IMG-20240409-WA0043.jpg
IMG-20240409-WA0045.jpg
IMG-20240409-WA0042.jpg
IMG-20240409-WA0044.jpg
 
Pigeni kura Ili wao wale.
Viongozi wa TANAPA wana maisha mazuri kufuru, wewe kapuku na shobo zako unahangahika kupigia kura vitu ambavyo vineshindwa kulikomboa taifa
 
Naipenda Kilimanjaro lakini Serengeti ipewe heshima yake aisee.
 
Ili wao waendelee kula? manina, Ukiangalia jamii tu zinazo zunguka hizo hifadhi kuna umasikini wa kutisha kabisa, nenda anagalia vijiji vinavyo izunguka hifadhi ya Serengeti.

Kwa kifupi hizi ni project za watu na siwezi piga kura bora huo muda nikaangalie hata cartoon youtube.
 
Pigeni kura Ili wao wale.
Viongozi wa TANAPA wana maisha mazuri kufuru, wewe kapuku na shobo zako unahangahika kupigia kura vitu ambavyo vineshindwa kulikomboa taifa
wacha wawapigie waendelee kula ajira zenyewe za kujuana. Huu ujinga sifanyi
 
Zile ngozi za Simba haewawajatupa majibu.
Yule mamba mkubwa wamepiga kimya Leo wanataka vote kumbvu zao
 
Naipenda Kilimanjaro lakini Serengeti ipewe heshima yake aisee.
Sijui ni ushamba au nini,nimetembea hifadhi nyingi ikiwemo Serengeti lakini Tarangire ni bonge la hifadhi.

Tarangire utawaona wanyamapori wengi katika eneo dogo sana wakati Serengeti utapuyanga mwendo mrefu bila kuona wanyamapori wa kutosha.
 
TANAPA wanapiga hela akuna taasisi inawafikia,narudia tena aipo taasisi inayopiga hela kuizidi TANAPA.

haya sawa ntapiga kura na mimi.
 
Sijui ni ushamba au nini,nimetembea hifadhi nyingi ikiwemo Serengeti lakini Tarangire ni bonge la hifadhi.

Tarangire utawaona wanyamapori wengi katika eneo dogo sana wakati Serengeti utapuyanga mwendo mrefu bila kuona wanyamapori wa kutosha.
Upo sahihi...Tarangire kupo vyema...wale (Zero Brain) Ngiri unapishana nao wakutosha wakikatiza barabara huku na huko.
 
Makusanyo yote ya hifadhi yanaenda direct hazina kupitia tra? Kama ni wa tanapa sidhani labda level za juu
Yanakwenda huko lakini sahani ya viongozi wa tanapa lazima ibaki au irudi na michuzi.
Watu wanapiga pesa mpaka hawajui wazifanyie nini wanabaki wanazijaza kwenye ndoo wanatunza ndani
 
Yanakwenda huko lakini sahani ya viongozi wa tanapa lazima ibaki au irudi na michuzi.
Watu wanapiga pesa mpaka hawajui wazifanyie nini wanabaki wanazijaza kwenye ndoo wanatunza ndani
Hilo nitakukatalia, miaka imebadilika sikuizi wanapewa gawio kutokana na mahitaji. Zamani ndio walikuwa wanaipa serikali gawio, sikuiz hawapokei hela mkononi,malipo ya hifadhi yanafanyika online , hiyo pesa wanaipata wapi wakati hawashiki hela mkononi?. So unaposema viongozi wake wanapiga , useme wanapigia wapi with facts
 
Back
Top Bottom