econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Wote wenye Nia ya kugombea nafasi za uongozi hasa uchaguzi wa nafasi ya Urais mwaka 2025 wajikite kwenye masuala ya Usalama na uchumi.
Kwanza, wajikite kwenye kuimarisha Usalama wa nchi. Hali sio nzuri kwa Sasa kutekwa na kupotezwa imekuwa Jambo la kawaida kwa Sasa. Inatakiwa Rais ajaye aweke mikakati maalum ya kuhakikisha raia wanalindwa na Wala hawapotei. Ni aibu sana tuna vyombo vya Usalama lakini Usalama wa raia umekuwa wa mashaka. Rais ajaye afumue jeshi la polisi na pia aweke standards kwa ma RPC kuhusu Usalama wa raia.
Pili, Rais ajaye aje na mbinu za kukuza uchumi wa Tanzania na kuongeza uzalishaji. Kwenye kukuza uchumi inatakiwa kwanza kushughulikia Deni la nje na namna gani tutalipunuza. Ili kupunguza Deni la nje inabidi Rais ajaye ahakikishe ya kwamba anaziba mianya ya rushwa na matumizi yasiofaa. Kwa mfano anaweza kufuta nafasi za wakuu wa mikoa na Wilaya kwa muda wa miaka mitano, halafu pesa zote ambazo zilikuwa ziende kwenye nafasi hizo zipelekwe kwenye kulipa Deni la nje. Pia mianya yote ya ufisadi izibwe kwa kutumia ripoti ya CAG ili mapato yapatikane kwa wingi na kiasi kitumike kulipia Deni la nje.
Ni muhimu pia wagombea wa urais mwaka 2025 waje na sera ya kukuza Ajira na kujiajiri. Ni namna gani wabunifu na wajasiriamali wa kitanzania watawezeshwa kukuza biashara zao na mitaji yao ndani ya nchi na nje ya nchi.
Uchaguzi wa 2025 uwe kwa ajili ya sera na sio mipasho na wasanii kwenye majukwaa. Tumchague Rais atakaye tuhakikishia Usalama wetu na kukuza uchumi wa Tanzania.