Mwanzoni nilifikiri amedondoka, na huyu binti anajaribu kumwinua. Maana hapo walipokaa pana mtelemko, na kofia ile ameidakia upande wa kushoto! Halafu nilipoona hio Bajaji nikapata mawazo tofauti labda ndio ameanza kutekeleza ahadi zake. Nikawa nimeguna kumbe naye huyu anaweza kuwa muungwana. Ikanibidi nimchunguze tena huyu binti kama ni mjamzito inaelekea hapana. Sasa kuna nini pale?
Nikakumbuka picha nyingine ya Raisi akiwa anaotesha mti, alipiga goti kwenye zulia ili aweze kuotesha mti. Hapa doh! amemshika binti kwa nyuma kwa mkono wa kulia, ana tabasamu la nguvu, miguu yote ameiacha hewani unaweza hata ukaona chochote alichokikanyaga kwenye viatu vyake.
Sasa nakuuliza Kingi, una maana hizi ndizo picha za kampeni za CCM! Acha bwana hawajachachuka kiasi hiki! Tumpe haki yake naye!