Ifuatayo ni ilani ya uchaguzi ya mgombea umakamo wa urais katika serikali ya DARUSO-DUCE. Hata kama wewe sio mwanduce ipitie uone jinsi huyu mtu alivyo hazina ya DUCE na hata jamii nzima ya kizazi kijacho. Mgombea mwenyewe ni MARTHA STEVEN (B.A. Education).
Hako katabia ka mtu kujitafutia uongozi ili apone njaa ni aina ya utamaduni mbaya kabisa. Kwa huyu mgombea ni tofauti tuna ushahidi hapa DUCE wa namna anavyojiingiza katika kutambua watu wanahitaji nini.