LGE2024 Kampeni za mtaa kwa mtaa kwa baadhi ya wanasiasa wa CCM mtaa wa Dovya kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa

LGE2024 Kampeni za mtaa kwa mtaa kwa baadhi ya wanasiasa wa CCM mtaa wa Dovya kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wakuu Kwema!

Leo nimekutana na moja ya mwanasiasa kutokea chama cha Mapinduzi ( CCM ) akijipigia kampeni kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Tunafahamu kwamba CCM wametangaza ratiba za wanachama wao kuanza kuchukua fomu kuzijaza na kurududisha na kuanza kampeni za ndani na ndipo wachaguliwe kwenda kupeperusha bendera ya chama hicho.

Sasa huku mtaani kwetu mtaa wa Dovya kata ya Bunju alijitokeza moja ya mwanasiasa kutoka CCM akitaka wananchi wa maeneo yale hususani wanachama wa CCM waende kumpigia kura za maoni ili jina lake lipite na hadi kufikia hatua ya kuwa mgombea rasmi wa chama hicho.

Ili kunogesha akawanunulia baadhi ya wamama vitumbua na soda pale kisha akaondoka zake.

Soma Pia: Tanga: CCM waanza kupiga kura za maoni kwa wagombea kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa

Sasa nikapata za ndanii kutoka kwa watu wanaomfahamu na kueleza kwamba anaugomvi na moja ya wagombea wenzie na wana bifu kali kweli.

Tahadhari kwa wananchi muda huu ni muda wa kulabwa miguu na wagombea tuwe makini kuanzia kura za maoni hadi kwenye uchaguzi wenyewe ili tupate viongozi wazuri zaidi.
 
Huku kwetu kuna mgombeq kapata kura moja na ana mke na watoto na wote wamepiga kura
 
Back
Top Bottom