Uchaguzi 2020 Kampeni za mwaka huu zitaiachia nchi nyufa za chuki, ubaguzi, dharau kwa dini na viongozi wake, hasira. Tunahitaji muafaka wa kitaifa

Benson Mramba

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2013
Posts
648
Reaction score
1,485
Baada ya kufuatilia kampeni za mwaka huu hususan za Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuangalia serikali na Tume wanavyochezesha mchezo huu wa kampeni nashuhudiwa ndani ya nafsi yangu kuwa iwapo CCM itashinda au CHADEMA tutakuwa na miaka mitano iliyojaa

1. Chuki baina ya Wananchi na Serikali na Wanachama wa vyama vikubwa vya siasa. Chuki hii inaletwa na upendeleo wa wazi dhidi ya CCM na kuzuia watu kutoa hasira zao waziwazi badala yake wanaweka vinyongo moyoni

2. Ubaguzi. Maadili ya Uchaguzi yanakataza matumizi ya lugha za makabila wakati wa kampeni. Bahati Magufuli anajua lugha za makabila mengi ya kanda ya ziwa na ameishi au kufanya kazi mikoa hiyo kwa wakati fulani. Sasa kampeni zake kanda ya ziwa ni kisukuma, kihaya n.k halafu yuko live TBC. Anawaonyesha kuwa yeye ni mwenzao ni mtoto wao. Hili ni ubaguzi na Mwl. Nyerere alisema hii ni sawa na kula nyama ya mtu. Magufuli, Bashiru, Polepole n.k wote kanda ya ziwa.

3. Dharau kwa Dini na viongozi wake. Kugombea kwa Askofu Gwajima na sala na dua wanazotoa viongozi wa dini kwenye kampeni za CCM ambazo ziko live kila siku zinafanya wananchi wengi tunawadharau matokeo yake tutadharau dini na mwisho wa siku kikinuka hatutakuwa na wa Kumsikiliza maana dini na viongozi wake tutaziona kama vyama tu.

Aidha hakuna kiongozi wa dini hata mmoja ambae amekemea au kuonyesha sympathy na Tundu Lissu hadharani dhidi ya shambulio lake la September 2017. Matokeo yake viongozi wa dini wanaelemea upande wa wawashukiwa wa tukio.

4. Hasira ipo dhidi ya uonevu. Itazidi sana wakati wa kutangaza matokeo na itachochewa sana na walioshindwa.

5. Kupoteza imani na sheria na vyombo vinavyoisimamia. Kama unaongea kwa lugha za makabila, unapiga simu kuagiza barabara zitengenezwe wakati uko kwenye kampeni kinyume na sheria inavyotaka na hatua yoyote inayochukuliwa hata ya onyo na wewe ndio Mkuu wa nchi maana yake unawaonyesha watu kuwa sheria haina maana au ni ya wale sio yako hali ya kuwa wakati huu wenzako nao wanakuchukulia uko kama wao ni shida.

Sioni kwa sasa katika serikali, dini au kwenye vyama mtu anayeweza kuzungumza na Taifa kwa umoja wetu. Tukiendelea hivi naona miaka 5 ya mivutano bila kufanya maendeleo. Tunahitaji Muafaka wa Kitaifa wakati huu wa kampeni kabla ya Kura na kabla ya Matokeo. Sioni upendo kati ya Magufuli na Lissu. Mafahali wawili wakivutana nyasi ndio zitaumia.

TUNATAKA MUAFAKA WA KITAIFA BARA NA ZANZIBAR KABLA YA SIKU YA KURA. JUKWAA LA WAHARIRI WAMEANZA KWA KUWAKUTANISHA CHADEMA NA TBC SERIKALI NAYO IFUATE KUPITIA TDC
 
Je hao ZEC wanaowazuia Wagombea hamuwasemi halafu baadae mnataka chuki ziishe chuki Tanzania zitaongezeka sana sana Magufuli atakuwa na nchi ngumu sana sijui kama anajua hilo anafikiri polisi na usalama wataweza atashangaa sana anamaliza miaka mitano akiwa na majonzi sana
 
Hongera sana kwa mada nzuri. Nakuona tu namna unavyojuta moyoni kwa sasa baada ya kuchagua unafiki katika umri wako huo mdogo ulio nao.

Ulitakiwa ubakie kwenye chama chako, mwanzo mwisho! Sisi kaka zako tunapoichukia CCM, hatukosei! Tuna sababu za msingi. Na kwa bahati mbaya wengi wetu tumeshindwa kuishi hayo maisha ya kinafiki uliyo yachagua wewe na baadhi ya wenzako.

Ila kwa ufupi, leo nimekuelewa sana. Katiba mpya ndiyo jibu la haya madudu yote tunayo yashuhudia sasa.
 
Naona umeanza kupata akili,

Sie wewe ulokuwa unasimama kidete na kudai Chadema na upinzani kwa ujumla ushakufa? Leo chama kilichojifia zamani kitamtetemesha vipi you aloleta maendeleo kila pembe ya Nchi hii? Mtu anaependwa na kuabudiwa na kila Mtanzania hapa Duniani anateseka vipi kwa kibaraka na ngumbaru wa Mabeberu?

Vijana mwache unafiki,

Kushadidia upuuzi na kuja kupinga upuuzi uleule baada ya kukosa teuzu ni ujinga mtambuka..!! Tuliza kipapo wenye maumivu ya kweli ya miaka mitano ya unyang'ani, mateso, kubambika na kila uovu ulotekea nchini hapa wapaze sauti za kilio cha kweli.. we tulizana.. huna Moral authority ya kuwa sauti ya wanyonge wa kweli ktk taifa hili.

BACK TANGANYIKA
 
Usinilishe maneno. Mimi nilikuwa napingana na Mbowe na kikundi chake namna ya uendeshaji wa Chama. Wanachama walinielewa. Sasa habari za Mbowe nimefunga. Niko na agenda nyingine.
 
Usinilishe maneno. Mimi nilikuwa napingana na Mbowe na kikundi chake namna ya uendeshaji wa Chama. Wanachama walinielewa. Sasa habari za Mbowe nimefunga. Niko na agenda nyingine.
Teh teh tehhhhhh...

Hebu pita hivi bhana... tusipotezeane muda. Ukimpinga Mbowe na kikundi chake ndo unaungana na watesi, wanyang'anyi na walaghai?

BACK TANGANYIKA
 
Umeongea mazito sana sana kwa mara ya kwanza. Huu uzi utaongoza kufuatiliwa baada ya uchaguzi.

Nikujuze tu; kwa mara ya kwanza UN itaingilia kati mizozo baada ya uchaguzi. Uchaguzi huu unafuatiliwa sana kuliko chaguzi zingine, inasubiriwa angalau watu 50 wapoteze maisha ili UN wapate sababu ya kuingilia kati.

Tusubiri.
 
Hali ni shwari kabisa mtoa mada, wewe chapa kazi mengine hayo ni kutaka kujaza watu hofu.

Baada ya tarehe 28/10/2020 maisha yataendelea na kama ilivyo kawaida CCM watakuwa wameshinda kwa kishindo.
 
Bushiri kawaambia vijana wake wajibu hoja za wapinzani ohoo wao wakaanza kuporokosha mitusi...na mbaya zaidi bora wangewatukana wanasiasa wenzao lakini wakaona ni vizuri waanze na hao viongozi wa dini.

Kweli hiki chama sasa si muelekeo tu Bali hata maadili hakina kabisa.
 
Katika watu wanoko na wenye chuki, roho mbaya, laana na nuksi ni wewe wa kwanza
Katika watu wajinga na wapuuzi wewe ni mmoja wapo ,Yani husomi kilichoandikwa wewe unakuja unacomment tuu,, hivi akili itapata lini?
 
Magufuli ni mbaguzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…