Uchaguzi 2020 Kampeni za mwaka huu zitaiachia nchi nyufa za chuki, ubaguzi, dharau kwa dini na viongozi wake, hasira. Tunahitaji muafaka wa kitaifa

Hawezi kuwa jiwe kwa sababu sifa ya jiwe ni kutokubadilika. Liko hivyohivyo enzi na enzi!!
 
Umetekwa au ni wewe mwenyewe umejituma ?
I mean that mwafaka wa kitaifa in those parameters is impossible. Resistance is inevitable. Infact it is the only alternative remaining on the table!!!
 
Policcm na Neccm ndio watakaovunja amani ya nchi hii , ng'ombe atachinjwa jinsi alivyolala ,hakuna kumpeleka kibla!! Policcm na nec wakitenda haki hakuna vurugu itkayotokea ila wakileta uhuni watapata wanachokitaka.

Viongozi wa Chadema ngazi ya jimbo washatoa tamko eg misungwi kwamba kuna vituo na wapiga kura hewa,kwahiyo janja ya NEC ishajulikana ,kila jimbo NEC watoe nakala ya matokeo kwa kila kituo na jumla yake ya jimbo iliflect kwenye nakala za mawakala yakienda tofauti lazima kinuke!! Hakuna upuuzi tena,tunatumia zaidi ya bil 600 kufanya uchaguzi halafu kumbe matokeo yapo mfukoni mwa NECCM si upuuzi huo? hizo b 600 si zingefanyie vitu vingine kama hamtaki uchaguzi huru? Mwaka huu mtajua hamjui,hakuna JANJA JANJA tena.
 
Nilisema na nitarudia...kwa namna ile ile Magufuli alivyosukumiziwa madaraka yaliyomzidi kimo, toka awali kabisa hakuona umuhimu wa kuwaomba radhi Watanzania kwa ushiriki wake katika kulifikisha taifa lilipofikia mwaka 2015.

Sio tu kwamba hakuona umuhimu wa kufanya hivyo, kwa kiburi cha ajabu alijifananisha na malaika aliyeshushwa tu kutoka sayari nyingine na kulikuta taifa lililopinda na lililo katika hali ya kusikitisha likihitaji mtu wa kulikomboa kama yeye.

Hakuishia hapo tu aliapa pia kuwalinda wote alioshirikiana nao kwa kipindi chote cha miaka zaidi ya ishirini kulifikisha taifa katika hali hiyo ya kusikitisha akiwataka walale bila hofu ya kuwajibishwa huku akidai kulinyosha taifa hilo.

Hakutaka ushiriki wala mapatano na wazalendo wa kweli ambao kwa miaka hiyo yote walikuwa wakipiga kelele wakati yeye pamoja na hao alioshirikiana nao wakineemeka kwa kutapanya rasilimali za taifa kama vile hazima mwenyewe.

Kwa miaka mitano aliyokaa madarakani alihakikisha anawanyamazisha wazalendo wote ambao hasa ndio walikuwa wahanga wakiteseka kwa hujuma zilizokuwa zikifanyika dhidi yao na genge lililotamba kuwa na hatimiliki ya taifa hili.

Katika miaka hiyo mitano kulikuwa kikundi kisicho rasmi cha wasiojulikana kilichotumika kuteka, kutesa na kuwapoteza wananchi ambao walikataa kuunga mkono juhudi hizo za kilaghai zilizoendeshwa kikatili kwa kivuli cha hapa kazi tu.

Na leo, kama vile kazinduka...

Katika wale waliolaghaiwa na hivyo kushawishika kuunga mkono juhudi hizo ovu, anatokea moja na bila hata kuwaomba radhi Watanzania waliopitia mateso makubwa ndani ya taifa lao, anatutaka tutafute muafaka na genge hilo...Benson Mramba, upo?
 
Tukubali tu kuwa mzee ndio anaanzisha hizi rafu wenzake wanamalizia.

Mzee anajisahau sana inapokuja swala la sheria na taratibu na kanuni mbali mbali za nchi. Kama viongozi wote wangekuwa na ujeuri wa kufanya vile wanavyojiskia bila kuheshimu au hata ka'aibu fulani kwenye sheria za nchi then sidhani kama taifa letu lingekuwa limesimama kama hivi.

Hili ni vema likazungumzwa na kukemewa wazi wazi pasipo kupiga chenga. Kwann tunakuwa ni watu wa kuonea haya au aibu kiongozi anapocheza na misingi ya taifa letu?!


Hebu tukemee hili na tukemee wazi wazi.
 
Usinilishe maneno. Mimi nilikuwa napingana na Mbowe na kikundi chake namna ya uendeshaji wa Chama. Wanachama walinielewa. Sasa habari za Mbowe nimefunga. Niko na agenda nyingine.
Mkuu, wewe si miongoni mwa walioshadadia kukamatwa kwa watu wanaovaa nguo iloandikwa "pray for Lissu"??
 

Kwanza ni kujua hali yako,maneno haya ni ukweli mtupu na hua mwanzo wa kutengeneza utengano wa kitaifa, hasa kama hakuta kuwa na matayarisho ya kukumbatiana.

Ila mnaniangusha Kilimanjaro, hasa Rombo, Hai na Vunjo safari hii mmeamua kuungama, nini kipya tena? Bi mkubwa nikizungumza nae na uncles wananiambia Lwamungo Sinde ya kijani. Nipashe kama kuna mpya.

Kila nikipata taarifa za huko napungukiwa ufahari na kuutingisha ujasiri wangu. Karibu sana na siku njema.
 
Mungu ashukuriwe kwa wewe kurudiwa na akili timamu umeongea jambo la msingi sana.

Tunaofahamu undani kidogo huyu yupo sawa tuu, ila Kaka alimpiga kofi la keleb akateleza, hivi anajitafuta tuu anarudi huyo, na mabadiliko yeyote ya juu kuna nondo za ukweli tutaungana kwa kurudi nyumbani. Siasa hizo ni suala la muda tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…