Kampuni binafsi ya uuzaji wa viwanja ina haki ya kuongea na kamishina wa ardhi ili wakufutie hati ya kiwanja?

Kampuni binafsi ya uuzaji wa viwanja ina haki ya kuongea na kamishina wa ardhi ili wakufutie hati ya kiwanja?

Joined
Sep 5, 2017
Posts
19
Reaction score
25
Wadao heshima yenu wakuu, naomba mnisaidie kupata mwanga juu ya swala Hilo, nmenunua kiwanja mwaka 2020 Kwa installments kwenye kampuni binafsi na nilikuwa nalipa Kashi pesa mkononi napewa risit za kuandikiwa na afisa masoko wa kampuni hiyo.

Baada ya kukamilisha malipo nilifatilia kupata Hati lakini walinisumbua sana wakachukuwa lisit zangu kuwa wanaenda kuziunganisha na documents nyingine Kwa ajili ya hati (nikazitoa kopi nikawapa hizo OG walizozitaka) usumbufu ulivyozidi nikafatilia Halimashauri mpaka nikaenda mwenyewe Halimashauri nikakamilisha taratibu zote.Nikafata Hati Wizarani.

Nmejenga na nyumba ipo kwenye linta

VIOJA VYAO

Hivi Sasa Kila kukicha Mkurugenzi wa kampuni hiyo anapiga simu akidai wameongea na KAMISHINA wataandika barua Hati yangu itafutwa Kwa sababu Afsa masoko akufikisha pesa Kwenye akaunti ya kampuni mara documents alifoji wanadai alinitapeli.

Afsa masoko yupo kampuni nyingine na anakili kuwa pesa haikufika lakini atailipa kampuni hiyo ya viwanja taratibu ila documents zote anadai ni sawa.

Kampuni hiyo ya viwanja wamekataa wananambia nisubir kufutiwa hati miliki ya wizara.

Naomba msaada wa kisheria nifate hatua Gani??

Natanguliza shukrani

Screenshot_20221202-132152.jpg
 
Mimi siyo mtaalamu wa sheria ila naona hapa ww hauna kosa kwa sababu una documents halali. Ningeshauri ikibidi mwende mahakamani. Wangekuwa sahihi kama wangemshitaki afisa masoko kwa kula hela yao na siyo kukusumbua ww
 
Sent from my SM-G965F using JamiiForums mobile app
Asante sana Kwa ushauri ndugu!

Na polisi tulienda wakashauriwa ivyo, ila Bado tu wananisumbua, nasubiria kuona barua Yao ambayo wanataka kunitumia,

Ili nipate kupata ushauri zaidi kujuwa Nihatua ipi niichukue,

Asante sana.
 
Wengi wapo vizuri ila mapungufu ya usumbufu ni baadhi ya kampuni akikisha unapata mikataba ambayo imesainiwa na mwanasheria
Mm nimepata mikataba toka mwezi wa 6 mwaka jana lkn mpka leo kampuni haitaki kunikabidhi viwanja vyangu kila siku ni ahadi tu. Na wanadai viwanja vya mwanzo vina mgogoro.
Je taratibu gani za kisheria naweza kufata nikapata haki yangu au wanirudishie pesa zangu.
 
Dah pole sana mkuu ni kampuni gan hizo zinafanya mambo sensitive hvyo kiholela...Yan viwanja vinamgogoro kivp wakati wanapswa kuhakikisha Kila kitu kimekaa sawa ndo wauze
 
Dah pole sana mkuu ni kampuni gan hizo zinafanya mambo sensitive hvyo kiholela...Yan viwanja vinamgogoro kivp wakati wanapswa kuhakikisha Kila kitu kimekaa sawa ndo wauze
Kampuni moja hivi ya real estate ipo manzese sema dawa yao ipo soon wataipata.
 
Kabla ya wizara kufuta hati lazima wakutafute na kujua Saba, wakiridhika wewe ni mkosaji wanapeleka taarifa kwa rais ili hati ifutwe.
Hiyo kampuni inakutisha lakini kuweka kumbukumbu sawa inabidi mawasiliano unayofanya nao yaweke kwenye maandishi.
Wao wanatakiwa kupambana na aliyekuwa pesa za kampuni.
Sijui risiti walikuwa wanakulipa za aina gani kama sio za efd wachome tra wanakwepa kodi
 
Back
Top Bottom