Kampuni Gani Waaminifu kuagiza Gari

muzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2016
Posts
1,041
Reaction score
1,457
Kama mada inavyojieleza ni kampuni gani nzuri, waaminifu, timely, kwenye kuagiza gari. Maana siku hizi kuna makampuni mengi, lakini tatizo linakuja wengine ni matapeli, wengine ni majizi, wengine utaagiza Fuso unaletewa Canter, wengine gari inakuja vitu vimechomolewa, wengine watakuambia hiyo gari ilishachukuliwa japokuwa wamekutumia invoice na ukalipa kwa wakati. Kwa sahivi kuna makampuni mengi kwa mfano BEFOWARD, SBT JAPAN, CARJUCTION,TRADECAR VIEW, TRUST JAPANIES VEHICLES, n.k
So kumekuwepo na matatizo mbalimbali kadha wa kadha kwenye uagizaji wa magari kutoka kwenye makampuni mbalimbali. Kwahiyo tushirikiane kwenye experience kuhusiana na kampuni ambazo wamekuwa waamifu kwa wakati, mali, pamoja na changamoto tulizopata kwenye uagizaji wa magari na kadhalika.
Kupeana experience itawasidia wengine kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza
Karibuni
 
Jaribu Real Car Japan, binafsi nimeona wana gari zenye low mileage halafu kwa bei nzuri sana tofauti na hao kina beforward gari kwao unakuta limekula kms laki na upuuzi ndio bei inakuwa ndogo.
Ushawahi kununua kwa hao Real Car Japan, wana local agent au branch hapa nchini?
 
Kuna mtu alii recommend jana, yeye ndie alinunua huko gari yake. Mi nilipitia kuona kunani ila so far nimevutiwa na deals zao. Gari ziko order na mileage ndogo halafu bei chee
Hao hao ndio Real motor japan au ni tofauti boss?
 
Mkuu nimenunua gari zaidi ya tano tradecarview ,hawana shida mkuu
 
Kuna mtu aliniambia kuna mitandao inafanya minada na unaweza pata kwa bei ndogo tofauti na kununua kwenye hiyo mitandao pendwa...bahati mbaya sina contacts za jamaa so kama kuna mtu anajua hiyo minada naomna atuwekee info hapa. Asante
 
Mkuu nimenunua gari zaidi ya tano tradecarview ,hawana shida mkuu
Jamaa wako expensive sana na bado unakuta miles zao ni za juu tu kama be forward though be forward wao ni cheap compared to Trade car view.
 
BEFOWARD na SBT Japan wanaushindani lakini katika yote bei ya BEWARD ni ndogo, kwa upande wa SBT Japan magari yao yametembea mileage nyingi sana na bado bei iko juu. Unaweza kuta gari kama Harrier ya 2015 ina mileage 220,000km sasa ukinunua hiyo japokuwa body inangaa lakini engine ishaanza kuchoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…