Kampuni inayoongoza kwa kugawa vyeo nchini!

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,636
Reaction score
2,728
Kampuni hii ni maarufu kwa jina la 'Alovera' ni kampuni yenye mameneja wengi kuliko kampuni yeyote nchini.
Ni kampuni nzuri kwa kusocialize huku una make money. Ni sehemu nzuri pia kwa kuuzia sura. Kwa wale ambao hawakufanikiwa kupata vyeo huko walipo hapa ni mahali pazuri pa kuupatia umeneja na kuweka CV yako vizuri. Hii ni mahali muafaka hasa kwa wale wenye elimu ndogo. Yapo mapungufu mengi kwenye hii kampuni but I dont want to dwell on that side kwa leo, ila moja kati ya hilo ni kuwa sijaweza kupima kiwango cha mafanikio cha 'mameneja' hao wa kampuni hii kama kweli hii biashara inaweza kukufanya ujenge nyumba, ununue gari kusomesha watoto n.k
Mtazamo wangu wa sasa naichukulia kampuni hii kama sehemu ya 'Kula na Kunywa' Mwenye wawazo tofauti na mimi anakaribishwa kuchangia humu jamvini. Sio mbaya ukitupia nyumba na magari ya wanachama ambayo wamenunua kutokana na biashara hii.
 
Used country new people

Msomi wa ktz ambaye kazi kubwa kujadili maisha ua wenginee
 
Ni strategies za soko tu,cku moja nilishangaa kumwona jirani yangu nae akitoa ushuhuda wa uongo kuhusu mafanikio yake!zaidi ya kuuza sura hakuna lolote ni machinga km wengine tu!
 
Ni strategies za soko tu,cku moja nilishangaa kumwona jirani yangu nae akitoa ushuhuda wa uongo kuhusu mafanikio yake!zaidi ya kuuza sura hakuna lolote ni machinga km wengine tu!

Duh, huyo jirani yako majanga!
 
Kama hamna taarifa za kweli kuhusu kampuni hii na nyingine zinazofanana na hizo ni bora mkakaa kimya tu...
 
Kama hamna taarifa za kweli kuhusu kampuni hii na nyingine zinazofanana na hizo ni bora mkakaa kimya tu...

Ndio maana tumewaalika watu kama wewe mtupe 'taarifa sahihi' kuhusiana na opportunity hii ya biashara.
Ni nafasi nzuri kwako kuandika na kutetea kile unachokiamini.
 
Ni vizuri ukatafuta taalifa sahihi na kuzitoa hapa.No research no right to say!hakuna cheo kinachopatikana bure pale. Nenda kajifunze utajua. Tatizo ni kwamba watu wamezoea huko duniani vyeo vinapatikana kwa kununua, kupendeleana, kuhonga n.k Kule hakuna kitu kama hicho ni juhudi zako tu. kila mtu ana fulsa sawa, uwe umesoma au haujasoma ili mradi umetimiza masharti. Usije ukadhani ukisoma sana ndiyo kigezo cha kufanikiwa. inaweza kuwa sivyo na kwa taalifa yako mapinduzi mengi ya kisayansi dunia hii yameletwa na watu ambao elimu za ni za kawaida sana. tafiti utaona hilo. Kuna mwandishi mmoja aliandika 'if you want to be rich don't go to school' unaelewa maana yake?
 
Unemployment ni zao la kukosa basic skills za production,taifa linapuuza kukomaza vyuo vyenye tija kama Sido na Veta matokeo yake ni kuwa na Graduates wasiokuwa na dira mitaani,hawa ndio wanageuka wahanga wa hizi kampuni za kiujanjaujanja za network marketing,ukiuliza endapo kila mtu akifanya hyo network marketing nani atamuuzia nan jibu hamna,haya haohao wanaojiita watu wa netwok marketing badala ya kuumiza vichwa na kuja na production yao wenyewe ya hzo food suppliments ili kuua ndege wawil kwa jiwe moja yani kutoa ajira na kujiajiri pia, bado wanategemea imported products ili wao watembeze kama MACHINGA na kutoa maneno mengi ya kuvutia watu...ndugu zangu inabd tubadilike sio lazima kuangalia mafanikio yetu binafsi kwamba ntaendesha gari na kujenga nyumba,lazima tufikirie ni namna gani tulifanye taifa lisonge mbele,mbona nchi nyingi za asia wameweza ku-buy class!..Tujikite kwenye uzalishaji binafsi otherwise taifa litageuka la WAMACHINGA...nb:wamachinga ni wachuuzi wa bidhaa wasizozitengeneza wenyewe.........My perspective kuhusu solution ya unemployment ni kuwa serikali ipunguze enrolment ya graduates badala yake watu wasomeshwe bure production na kisha wapatiwe vitendea kazi baada ya kuhitimu,few years to come tutaanza kuexport bidhaa za mbao kama meza na kabati badala ya ilivyo sasa, unatakiwa ujisikie aibu ninapokuuzia ugali wakati mahindi nimenunua kwako!..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…