Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 26,961
- 77,890
Tesla wametoka kutangaza robotaxi zao Cybercab na Cybervan juzi, Sasa Baidu nao kutoka China wamejibu kwa kutukumbusha kua wapo hewani na wameongeza gari lao jipya lenye full autonomous self driving.
Baidu (kama Google ya China) ni kampuni la teknolojia kutoka China wao wameanza delivery ya gari la wanalodai ni bora kuliko Cybercab, litakalo uzwa kwa $29,000 tu.
Yichi 06 ni electric minivan iliotengenezwa na JMC wakishirikiana na Apollo, huku Baidu akitoa huduma ya software.
Kwa muonekano, tofauti na Cybercab yenyewe ina seat nne.
Hakuna steering wheel, ila inaendeshwa na 6 generation ya Apollo autonomous driving system, ambayo ni Level 4 na 5 ADAS.
Upande wa hardware gari ina sensors 40 zikiwemo LiDAR tano zitakazosaidia autonomous driving.
Ina electric motor moja inayotoa horsepower 147 iliyopo mbele (FWD). Ina battery la LFP ambalo wamedai unaweza li-swap kwa dakika 3 tu katika swapping station.
Hadi sasa Baidu wanaendesha robotaxi China tu na wameshakamiliza zaidi ya rides million 7 au jumla ya Kilometa Mil 32 kwa huduma yao. Ila juzi tar 09 kwenye Presentation walisema wameshaamza kupata vibali vya kuingia nchi nyingine.
Tesla amesema yeye Cybercab zitaanza kazi 2026, as if Wachina wanamsubiria.