Kampuni kutoka China Baidu wameanza delivery ya Robotaxi yao Yichi 06, isiyokuwa na steering wala Pedal

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Tesla wametoka kutangaza robotaxi zao Cybercab na Cybervan juzi, Sasa Baidu nao kutoka China wamejibu kwa kutukumbusha kua wapo hewani na wameongeza gari lao jipya lenye full autonomous self driving.



Baidu (kama Google ya China) ni kampuni la teknolojia kutoka China wao wameanza delivery ya gari la wanalodai ni bora kuliko Cybercab, litakalo uzwa kwa $29,000 tu.



Yichi 06 ni electric minivan iliotengenezwa na JMC wakishirikiana na Apollo, huku Baidu akitoa huduma ya software.


Kwa muonekano, tofauti na Cybercab yenyewe ina seat nne.
Hakuna steering wheel, ila inaendeshwa na 6 generation ya Apollo autonomous driving system, ambayo ni Level 4 na 5 ADAS.

Upande wa hardware gari ina sensors 40 zikiwemo LiDAR tano zitakazosaidia autonomous driving.

Ina electric motor moja inayotoa horsepower 147 iliyopo mbele (FWD). Ina battery la LFP ambalo wamedai unaweza li-swap kwa dakika 3 tu katika swapping station.

Hadi sasa Baidu wanaendesha robotaxi China tu na wameshakamiliza zaidi ya rides million 7 au jumla ya Kilometa Mil 32 kwa huduma yao. Ila juzi tar 09 kwenye Presentation walisema wameshaamza kupata vibali vya kuingia nchi nyingine.

Tesla amesema yeye Cybercab zitaanza kazi 2026, as if Wachina wanamsubiria.
 
Nilisoma mahali autonomous driving system zinategemea pia sensors za barabarani ku operate. Leo nimetafuta info ili ku verify sijapata chochote cha maana. Mad Max any insight please
 
Mad Max kuna FALA Fulani na mada yake ya kifala nimemwambia kuwa wachina kwenye hii technology ya autopilot wanayo muda mrefu bado amekuwa mmbishi ...Kwa kifupi technology ya mchina ni nafuu kwa watu wote duniani tofauti na USA.

Tesla zitauzwa Kwa matajiri Tu ila kampuni za kichina zitaendelea kuuza Kwa volume kubwa Sana hasa Kwa Asia, Australia, south America na Africa
 
Nilisoma mahali autonomous driving system zinategemea pia sensors za barabarani ku operate. Leo nimetafuta info ili ku verify sijapata chochote cha maana. Mad Max any insight please
Mkuu.

Gari kujiendesha zinategemea tu hardware na software ya gari.

Hardware ni pamoja na sensors, radars na camera.

Software itategemea kila gari wanayotumia mfano Tesla yeye ana FSD na anakua anaiupdate kila muda.

Sema alama za barabarani zitakua zinasomwa na izo camera mfano Zebra, speed limits, traffic light nk.

Changamoto kwa barabara kama zetu unakuta mistari ya chini imefutika, trafiki anakaa yeye badala ya taa, kuchomekeana kwa bodaboda nk.
 
Nilisoma mahali autonomous driving system zinategemea pia sensors za barabarani ku operate. Leo nimetafuta info ili ku verify sijapata chochote cha maana. Mad Max any insight please
Mostly ni
proximity sensors for obstacle avoidance (radar, ultrasonic, photoelectric, etc)
Human/animal detection - infrared sensor
sound sensors for voice recognition
Camera sensors for image and live video processing, situation awareness using Deep neural network, road signs turns, zebras, traffic lights,
Live Google Map for street view, destination tracking, etc
 
Yeah goals za Tesla na goals za Wachina ziko tofauti kabisa na ndio inawasumbua Tesla sahivi.

Tesla tuseme kama Apple, anazingatia exclusivity ya bidhaa zake ndio maana hadi leo hataki kuleta cheap Tesla.

Wachina wao wanaangalia cheap ili kila mtu aweze kumiliki.

EV mbali na environmental friendly watu wanafikiria issue ya cheap running and maintenance cost.

Sasa unaniletea gari la $130,000 Cybertruck unategemea mtu atanunua wa chini?

Xi Jinping anajua balaa la Mchina kwenye technology ya autonomous. Wameanza kitambo sana tena kwa Level 3 kwenda juu.

Tesla juzi tu ndio amepata goahead ya Level 3 zamani ilikua Self Driving ila Supervised.
 
Nilisoma mahali autonomous driving system zinategemea pia sensors za barabarani ku operate. Leo nimetafuta info ili ku verify sijapata chochote cha maana. Mad Max any insight please
Ni kweli waataalumu wanasema ili autonomous driving systems iwe salama kabisa.
Ina bidi magari hao yawe na njia zake pekee, kama ilivyo mwendo Kasi hapa Bongo.
 
Gari zinazojiendesha zenyewe hata marekani zipo kwenye baadhi ya majimbo.
 
Namna hii haitakuwa ngumu sana ku operate Afrika. Ndio concern yangu kubwa
 
Ni kweli waataalumu wanasema ili autonomous driving systems iwe salama kabisa.
Ina bidi magari hao yawe na njia zake pekee, kama ilivyo mwendo Kasi hapa Bongo.
Logical. Kuna situations zinahitaji reaction ya binadamu tu, especially huku kwetu
 
Gari zinazojiendesha zenyewe hata marekani zipo muda mrefu tu kwenye baadhi ya majimbo kama San Francisco.
 
Gari zinazojiendesha zenyewe hata marekani zipp muda mrefu tu kwenye baadhi ya majimbo kama San Francisco.View attachment 3122628
Yeah Waymo zamani Google ila wao hawana magari kama Tesla ila wanaingia mkataba na kampuni la magari.

Yaani Waymo ni kama Uber au Bolt., mkukubaliana wana install software na hardware zao kwenye gari lako.

Ndio maana magari yao kwa juu yana komwe flani.
 
Karibu nusu ya Tesla zinatengenezwa China

Jipe Moyo panda driveless cars za China..!!

Ushasema Tesla hata kama inatengenezwa China, but its highest Technology and proven reliability built unquestionable trust to customers, but not Chinese..!!

Chinese hata gari za kawaida bado shida au ndege zao hakuna za abiria, alafu iwe driver less cars?
 
Kuna magari yana quality kubwa sana huko.
 
Huko wamepita sasa wako kwenye ndege ya kukodi itakayokufuata mtaani kwako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…