Limited company huwa na Memorandum and Articles of association ambapo ktk hiyo memorandum kuna kuwa na objectives za hiyo company, wakurugenzi na share holders,pia mtaji wa hiyo company.
Kwa Tanzania Brela ndio wanasajili company na gharama za usajili zinatofautiana kutegemeana na mtaji uliondikwa kwenye Memorandum and Articles of Association.
Mtaji wa chini zaidi ni 1,000,000 na brela kulipia usajili utatakiwa kulipa 187,200 kama memorandum zikiwa 5 , na mtaji wa juu yaani zaidi ya mil 50 na kuendelea brela watataka ulipe 532,200 kama memorandum zikiwa 5.
Businessname hizi huweza kuwa na neno company Ila haziwezi kuwa limited. Mtu mmoja au kikundi kisichozidi watu 20 wanaweza kusajiliwa brela kwa gharama ya 20,000
NB kuna gharama nje hizo za brela utatakiwa kuwalipa watalaamu wakusaidie kuandaa na kugongewa muhuri wa wakili kwa upande wa limited company