Hizi hafla hafla hizi zimezidi. Kwani kuna ulazima gani wa kufanya hafla ili kukabidhiwa leseni?
Yaani kitu ambacho kinatakiwa kitumwe kwa posta au kiende kuchukuliwa ndani ya mfuko wa kaki kinafanyiwa sherehe na viongozi wanaenda kusherehekea...... Naona amekosa mkasi tu kukata ribbon ya uzinduzi!!!
Tanzania tuanze kulipwa kwa masaa!!! Mtu uki clock-out ndani ya masaa ya kazi unaenda unpaid.
Yaani kitu ambacho kinatakiwa kitumwe kwa posta au kiende kuchukuliwa ndani ya mfuko wa kaki kinafanyiwa sherehe na viongozi wanaenda kusherehekea...... Naona amekosa mkasi tu kukata ribbon ya uzinduzi!!!
Tanzania tuanze kulipwa kwa masaa!!! Mtu uki clock-out ndani ya masaa ya kazi unaenda unpaid.
Imetolewa mara ya mwisho: 22.11.2008 0003 EAT
Kampuni mbili mpya za simu za mkononi zaingia
Na Eben-Ezery Mende
Majira
KAMPUNI mbili mpya za simu za mkononi zimepewa leseni kwa ajili ya kutoa huduma hizo na kuungana na nyingine kubwa nne zilizopo hivi sasa.
Zilizopewa leseni hizo jana na Mkurugenzi wa Mamlaka Mawasiliano nchini (TCRA), Profesa John Nkoma, ni Mycell na Egotel.
Pamoja na kampuni hizo, kampuni nyingine ya Zain ilipewa leseni ya kutoa huduma zake kimataifa baada ya kuwa na leseni ya huduma za ndani tangu mwaka jana.
Akikabidhi leseni hizo Dar es Salaam Profesa Nkoma alisema Zain imefikia hatua hiyo ya kuingia katika ushindani wa kimataifa baada ya kujiimarisha kimasoko.
Alisema kuwapo na ongezeko la kampuni za mawasiliano kumeongeza ushindani wa kibiashara na utasaidia kupunguza gharama za mawasiliano kwa wateja.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa leseni hiyo, Mkurugenzi wa Mycell, Bw. Yusuf Manji ambaye pia ni Mkurugenzi Mrendaji wa kampuni ya Quality Group, alisema kampuni yake imejizatiti kutoa huduma ya mawasiliano kwa kiwango bora kinachokubalika katika tasnia ya mawasiliano.
Naye Mkurugenzi wa Egotel, Bw. Mohamedi Ali, alisema soko la ushindani la mawasiliano ni kubwa nchini, lakini bado linahitaji uwezo mkubwa wa huduma hiyo.
Kampuni zingine zinzotoa husuma hiyo ya simu za mkononi ni pamoja na Tigo, Vodacom na Zantel.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA),
Profesa John Nkoma (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi
wa Kampuni mpya ya simu ya Mycell, Bw. Yusuph Manji
leseni ya biashara katika hafla iliyofanyika, Dar es
Salaam jana. Anayeshuhudia ni Ofisa Mawasiliano wa
TCRA, Bw. Victor Nkya. (Picha na Charles Lucas)
Hapo cha kilichotiliwa mkazo kwenye hizo sherehe sio kutolewa kwa hiyo leseni, bali ni "mtu" anayepewa leseni.
Mimi nimefurahi thou..wacha wafungue makampuni ya simu lukuki, washindane weee sie walala hoi tutanufaika na gharama nafuu za kupiga simu.
Ila I wish kama wangekuwa wanatumia minara ya kurusha mawimbi ya simu kwa kushirikiana, badala ya kila kampuni kujenga minara yake.
Manji kweli kiboko mpaka anafungua kampuni ya simu?
Au wapo share na vibopa wa serikalini?Ngoja tusubili tutapata news.
Minara haina deal tena, mwakani tutakuwa tunazungumzia fibre optic cable panapo majaliwa
Nilishawahi kulifikiria hilo wazo before mkuu, kumbe siko pekeyangu. Zile Lunch zoote za saa sita mpaka saa nane mchana wakati huo huo ulikuwa na breki fupi ya supu asubuhi, halafu ikifika saa tisa na nusu huyooo kibegi kwapani siku imekwisha huu mchezo wa kizembe na ufe......Tanzania tuanze kulipwa kwa masaa!!! Mtu uki clock-out ndani ya masaa ya kazi unaenda unpaid.
Mukulu,hii FIBRE OPTIC CABLE ni kitu gani unaweza kulete msaada hapa kwa sisi tusio jua tafadhali.