Kampuni tatu zilizopo katika soko la hisa zilizofanya vizuri mwaka 2023

Kampuni tatu zilizopo katika soko la hisa zilizofanya vizuri mwaka 2023

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
kwa mwaka 2024 ,Soko la Hisa la Dar lina jumla ya makampuni 25...kutoka 27
kampuni 1 lilifirisika na kuondolewa sokoni....YETU MICROFINANCE
Kampuni moja limenunuliwa na kampuni lenzake......TWIGA CEMENT kainunua kampuni ya SIMBA CEMENT

Ila hauna uwezo wa kununua makampuni manne ,ambayo ni makampuni ya ya Kenya
KCB,NMG,EABL na JUBILEE Holdings,nafkiri kwasababu ya kuogopa makampuni ya Kenya kuja kuteka soko ,kwani wao wame tuzidi.
Lakini mpaka sasa ni makampuni 6 tu ambayo nimeona wameshachapisha taarifa zao za fedha za mwaka 2023.
Makampuni matatu ambayo kwa uchambuzi wangu naona ni bora na yamefanya vizuri ni....

3.DSE-DAR ES SALAAM STOCK EXCHANGE
Hii ndiyo kampuni inayoendesha soko la hisa.
  • wanaongoza kwa kuwa na Amali za kutosha za kulipa madeni yao yote na bado wakasimama.
  • wanarudisho zuri la faida kwa wanahisa na uwekezaji
  • wametoa gawio zuri
2.CRDB
  • Imeongoza kwa kutengeneza faida,zaidi ya billioni 370
  • ndiyo imetoa asilimia kubwa ya gawio kwa hisa....11%
  • ila inaangushwa na kiwango cha madeni kwa amali zake
1.TWIGA CEMENT
Hili ndiyo kampuni bora kwa mwaka jana ,na sidhani kama kuna kampuni litakuja kulipita.
  • Ilifanikiwa kuinunua kampuni yenzake ya saruji,SIMBA CEMENT
  • Ya pili kwa kutoa gawio kwa hisa
  • ina ongoza kwa uwiano mzuri wa faida kwa kila hisa unayo miliki...

Hii ni kulingana na uchambuzi wangu,
Ki taaluma mimi nahusika na uhandisi ujenzi,ila katika mda wangu wa bure huwa natumia kufuatilia masuala ya masoko ya mitaji....
kwa wale wana uchumi muliopo humu...naoma tusaidiane.


pitieni hiyo EXCEL FILE
password: JAMII
 

Attachments

Back
Top Bottom