Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Bangladesh inakusanya malipo ya kampuni ya umeme ya Adani baada ya kampuni hiyo ya India kukata usambazaji wa umeme, huku ikiripotiwa kuwa ni kutokana na malipo ambayo hayajalipwa ya dollar $800m.
Maafisa wawili wakuu wa serikali waliiambia BBC kuwa tayari wanashughulikia baadhi ya malipo ya kampuni ya Adani, ambayo hutoa 10% ya umeme unaotumiwa na Bangladesh.
"Tumeshughulikia matatizo ya malipo na tayari tumetoa mkopo wa $170 milioni [£143m] kwa kampuni ya Adani," afisa mkuu wa Bodi ya Umeme ya Bangladesh aliambia BBC.
Kampuni ya Adani huipatia Bangladesh nguvu za umeme kutoka kwa kiwanda chake cha megawati 1600 kinachotumia makaa ya mawe mashariki mwa India.
Hata hivyo, kampuni hiyo haijajibu maswali ya BBC kuhusu kupunguzwa kwa usambazaji wa umeme kwa Bangladesh, ambayo inakabiliwa na uhaba wa umeme mara kwa mara.
Maafisa wanasema kampuni hiyo imetishia kusitisha usambazaji kabisa ikiwa pesa inayodai haitaikuwa imelipwa kikamilifu kufikia tarehe 7 Novemba.
Karibu sana Tanzania Adani tumesimuliwa mambo mazuri na viongozi pamoja na wanasiasa. Ila kama tu Bangladesh wameanza kuumia sijui Tanzania tunasubiria nini?
Soma: Adani Group kutumia Tsh. Trilioni 2.4 kuwekeza kwenye Umeme Tanzania