ndiyomkuusana
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 666
- 426
Na Beatrice Shayo
23rd February 2013
Kamati inayoshughulikia Uigizaji wa Mafuta kwa Pamoja nchini (PIC), imeisimamisha kampuni ya Addax Energy SA ya Geneva nchini Uswis kutokushiriki kwenye mchakato wa zabuni nne za uigizaji mafuta ya jumla kufuatia sakata la kuleta mafuta chini ya kiwango.
Kampuni hiyo hivi karibuni iliingiza nchini tani 100,000 za dizeli kwa meli ya MT AL Buraq lakini Shirika la Viwango nchini (TBS), iliyazuia mafuta hayo kupakuliwa kutokana na kuwa chini ya viwango vya ubora hivyo kutofaa kwa matumizi.
Baada ya mafuta hayo kuwasili nchini, kabla ya kupakuliwa TBS iliyakagua na ndipo ilipobaini kuwa chini ya viwango na kuamuliwa yarudishwe yalikotokea nchini Uswis kwa kuwa makubaliano ya mkataba yalikiukwa.
Mafuta yaliyorudishwa yalitakiwa yatumike kwa kipindi cha Desemba hadi Januari 5 mwaka huu.
Akizungumza na NIPASHE Jumamosi jana jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa PIC, Michael Mjinja, alisema mshindi wa zabuni ya tisa ya uigizaji mafuta kwa mwezi Machi mwaka huu ilikuwa ni kampuni ya Gapco Tanzania Limited.
Mjinja alisema tayari kampuni hiyo ya Addax Energy imechukuliwa hatua kali kwa mujibu wa mkataba ambapo wametakiwa kulipa fani ya dola 0.5 kwa tani za ujazo.
Hata hivyo, Mjinja alisema mbali na adhabu hiyo, waisimamisha kushirika katika zabuni nne za uigizaji wa mafuta ya jumla kuanzia Februari mwaka huu na pia kurudisha fedha zote za makato ya benki. Alisema adhabu hiyo huenda ikafika hadi Julai kwa kuwa tayari.
Kuhusu mchakato wa zabuni ya tisa ya uigizaji mafuta, Mjinja alisema kampuni nane zilichukua fomu na kampuni sita ndizo zilirejesha nakala.
Alizitajakuwa ni Augusta Energy S.A, Enoc Africa Limited, Gapco Tanzania Limited, Glencore Energy Uk, Gunvor SA na Vitol SA Switzerland.
Mjinja alisema kampuni ambayo imeonyesha kiwango cha chini ni Gapco Ltd ambayo ni 46.5 huku kiwango cha juu kikionyesha 56 kwenye masuala ya primiamu.
Alisema kampuni hiyo itaanza kuleta mafuta ya petrol kati ya Machi 23 hadi 25 mwaka huu na dizeli kuletwa machi 18 hadi 20.
Hata hivyo, Mjinja alisema hali ya mafuta nchini inaendelea vizuri na meli zinaendelea kuleta mafuta na pia kuna akiba ya kutosha.
Alisema tenda hiyo ambayo ilikuwa itangazwe Januari 31 ilifutwa kutokana na kwamba kampuni hizo zilikuwa zimekosea ujazaji wa nyaraka, hali ambayo ingewaletea matatizo katika kusainisha mkataba.
Hata hivyo, alisema kusimama kwa zabuni hiyo hakuna madhara kwani yapo mafuta ya kutosha.
Alisema kwa siku mafuta ya petroli hutumika lita milioni 2, diseli lita milioni 3.9, mafuta ya ndege lita 550,000 na mafuta ya taa 190,000.
CHANZO: NIPASHE