A
Anonymous
Guest
Kampuni hiyo imekuwa na viongozi wenye ‘blabla’ nyingi, wanatoa ahadi ahadi mbalimbali za kulipa tena kwa maandishi lakini imeshindikanika kutimiza.
Tunaowadai kila mtu ana madi yake tofauti, wapo wanaodai malipo ya Miaka Miaka 4 na wengine zaidi, uzoefu unaonesha ili ulipwe inatakiwa uende pale na kuweka shinikizo sana ndipo watakulipa.
Tukakubaliana kuwa malipo ya kundi la kwanza yaanze kufanyika Julai 2024, hata hivyo malipo haya hayakufanyika.
Ilielezwa kuwa Serikali imesitisha malipo hayo kwa kumteua meneja usimamizi wa kampuni hiyo ili kuchunguza madai hayo.
Hii sio mara ya kwanza viongozi wa Serikali kuingilia kati suala hili la malipo yetu kila tunapokaribia kulipwa. Kuna taarifa kuwa Kampuni ya IGT inamilikiwa na vigogo Serikalini wanaotumia nguvu yao kulizima suala hili.
Baadhi ya wadai ni wazee, wengine wana Watoto wadogo, wengine wanavyuma katika maungo yao vinavyotakiwa kutolewa kwa gharama, maana kwa sasa si tiba tena ila ni ugonjwa.
Kama Serikali inasisitiza kuhusu ulipaji wa malipo ya Bima, kampuni zenyewe za bima zinafanya mambo kama haya, hii sio sawa.
Majibu ya TIRA kuhusu mgogoro huo ~ Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) yaingilia kati mgogoro wa Kampuni ya Bima ya IGT kushindwa kulipa madeni