Kampuni ya China Greely, yanunua hisa nyingi kwenye Mercedes-Benz

Kampuni ya China Greely, yanunua hisa nyingi kwenye Mercedes-Benz

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
benz.jpg

Kampuni ya kuunda magari ya China Geely, imekuwa mwekezaji mkubwa kwenye kampuni mmiliki wa magari ya Mercedes-Benz, Daimler, ikisema ina matumaini ya kushirikiana na kampuni hiyo kubwa ya Ujerumani katika kuunda magari ya yanayotumia umeme.

Hisa za Geely zilipanda huko Hong Kong baada ya makubaliano ya kununua asilimia 10 ya kampuni ya Daimler kutangazwa wikendi.

Kampuni hiyo ya China tayari inamiliki kampuni yote ya kuunda magari ya Sweden, Volvo.
Mwenyekiti Li Shufu anatarajia kukutana na maaafisa wa Daimler leo Jumatatu na maafisa wa serikali ya ujerumani baadaye wiki hii.

China inaaminika kwa na soko muhimu zaidi duniani kwa makampuni ya kuunda magari.

Katika taarifa ya Greely, Bw Li alisema anataka kuandamana na Daimler katika kuwa kanpuni kubwa zaidi kuunda magari wa umeme duniani.

Pia mwishoni mwa wiki, Daimler ilitangaza dola bilioni 1.9 za kuwekeza katika ushirikiano na kampuni nyingine ya magari ya China BAIC.

Pesa hizo zitatumiwa katika kuboresha kiwanda cha BAIC cha kuunda magari ya Mercedes yakiwemo yanayotumia umeme.

Wiki iliyopita kampuni nyinginje ya Ujerumani ya BMW ilitangaza maafikiano na kampuni ya China, Great Wall Motor, kununua magari ya umeme kwa soko la China.

Chanzo: BBC Swahili
 
haya makubaliano hayajashusha bei ya hisa za mercedes benz? Kwa sababu China wanasifika kwa takataka
 
Mercedes Benz wanalinda vipi jina lao hasa kwenye ubora wa magari yao maana China wao wanajali soko tuu na sio ubora sana
 
naona china anakila nia ya kukamata soko la ulaya akifuatiwa na India maana Tata wako mbio sana
 
Sasa mtu mwenyewe una laki unusu kisha unataka TV ya inch 60 kama Samsung au Lg, kwanini wasikuuzie ya ovyo?

Pesa yako unayolipa ndio ina determine quality ya bidhaa.
kuna uelewa tunatofautiana mkuu unaweza kwenda kariakoo na 650,000 yako unataka tv inch 32 na badl ukauziwa feki!!
kama kusingekua na bidhaa feki sokoni ingekua poa sana
 
kuna uelewa tunatofautiana mkuu unaweza kwenda kariakoo na 650,000 yako unataka tv inch 32 na badl ukauziwa feki!!
kama kusingekua na bidhaa feki sokoni ingekua poa sana
Sifikirii kama ni kosa la wachina wewe ukinunua TV 650,000 ambayo ilitakiwa iwe original lakini ukapewa feki. Nafikiri ni kosa la anaekuuzia alitakiwa akwambie kama hii feki. Mana uko china ata madukani unaambiwa hii ni feki.
 
Sifikirii kama ni kosa la wachina wewe ukinunua TV 650,000 ambayo ilitakiwa iwe original lakini ukapewa feki. Nafikiri ni kosa la anaekuuzia alitakiwa akwambie kama hii feki. Mana uko china ata madukani unaambiwa hii ni feki.
inahitaji moyo. sana kumwambia Mtej hii bidhaa ni feki!!
mara nyingi utasikia "hii ndo toleo jipya"
 
Sijui kwanini watu wako bize na feki au original wanasahau kuangalia China inavyopaa
 
Kwanini Tanzania haipai kama China?
Kwa sababu kuna hiki kitu cha viongozi wetu kutokua na dira na kutoifuata.

Mfano sasa hivi tumeambiwa uchumi wetu uwe wa viwanda lakini hakuna maandalizi ya kuvifikia viwanda.

Hatukuwahi kuwekeza kwenye kilimo ili tuwe na malighafi.

Hatukuwahi kuwekeza kwenye wataalamu.

Hatukuwahi kuwekeza kwenye teknolojia.

Kwahiyo ingawa kwenye kuandika ni rahisi ila kwenye practice sera ya viwanda ina asilimia kubwa za kufeli.

Tofauti na China, walifanya Great Leap Forward, jngawa yalikua mapinduzi ya kilimo yaliyoua watu wengi ila ndiyo msingi wao ulipoanzia.

Kingine ufisadi, tunawalea sana mafisadi. Nimesahau mwaka ila China waligundua kuna waziri kapendelea tenda kwa mtu ambaye hakustahili kushinda lakini hiyo kampuni ni ingetengeneza treni yenye spidi dunia nzima.
Yule waziri aliuawa.
 
inahitaji moyo. sana kumwambia Mtej hii bidhaa ni feki!!
mara nyingi utasikia "hii ndo toleo jipya"
Hao sio wauzaji waaminifu. Kule china unaambiwa kabisa kama hii kitu sio yenyewe, na unaulizwa kama unataka wakubandikie logo ya kampuni unayotaka.

Anatakiwa akwambia kama hii sio yenyewe, angalau akwambie hii ni grade ta chini kidogo tu kulinganisha na yenyewe.

Na Tv sijui kuna namna gani kuitambua feki au yenyewe, mana angalau simu utasikia sijui bonyeza namba fulani sijui nini....
 
Back
Top Bottom