Kampuni ya FIC imenitapeli. Naombeni Ushauri

Kajeba

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2020
Posts
1,057
Reaction score
2,364
Kampuni ya FIC Imenitapeli – Naombeni Ushauri

Ndugu wanajamii,

Nimejikuta katika hali ngumu baada ya kuwekeza zaidi ya shilingi milioni 1 katika kampuni ya FIC, lakini sasa fedha hizo hazipatikani. Nimejaribu kutoa bila mafanikio, na sijapata majibu ya kuridhisha kutoka kwa kampuni husika.

Naomba ushauri wenu:
  1. Je, kuna mwanajamii mwingine aliyekutana na tatizo kama hili na FIC? Kama ndiyo, ulitatua vipi?
  2. Nini hatua sahihi za kuchukua katika hali kama hii? Je, ni vyema kuripoti kwa vyombo vya sheria au kuna njia nyingine za kutatua suala hili?
  3. Kuna taarifa zozote kuhusu uhalali wa kampuni ya FIC nchini Tanzania? Je, imesajiliwa rasmi na mamlaka husika?
Ningependa kusikia mawazo na ushauri wenu ili kujua hatua gani zichukuliwe katika hali hii.

Asanteni.
 
Hua mnaanza kuwekeza , mnaanza kujiita mabilionea mna michongo mingi , .mnapanga kununua viwanja vya mabilioni, magari ya kifahari , mnaanza kudharau watu , baadae mwisho kabisa mnapigwa kama wendawazimu mnaanza kuugulia maumivu
 
Pole mtumish ushapigwa

Biashara ni huduma na bidhaa

Full stop
Business= goods and services in exchange to money. Japo hata kwenye biashara pia watu hupigwa vilevile Nigerians , wapopo Wana platforms kibao za mauzo ukilemaa unapigwa na bidhaa zako au unatumia bidhaa unaambiwa iko chini ya kiwango wao hawawezi kuichukua usubiri wakuuzie , utasubiri hadi uchoke na uchakae, kitu cha kibiashara unaona kabisa mbona matajiri wakubwa hawapo huko wewe unahisi ni mchongo tena unafanya Siri kumbe dunia inakuona boya Tu kama maboya wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…