Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kampuni ya Jamhuri Media Limited, wachapishaji wa Gazeti la Uchunguzi JAMHURI inapenda kuufahamisha umma kuwa katika kikao cha pamoja kilichofanyika Aprili 29, 2020 kati ya wafanyakazi na mwajiri; tumekubaliana kupunguza asilimia 50 ya wafanyakazi kwa utaratibu maalum kuepusha kampuni isianguke.
======
Aprili 29, 2020
TAARIFA KWA UMMA - KUPUNGUZA ASILIMIA 50 YA WAFANYAKAZI
Kampuni ya Jamhuri Media Limited, wachapishaji wa Gazeti la Uchunguzi JAMHURI inapenda kuufahamisha umma kuwa katika kikao cha pamoja kilichofanyika Aprili 29, 2020 kati ya wafanyakazi na mwajiri; tumekubaliana kupunguza asilimia 50 ya wafanyakazi kwa utaratibu maalum kuepusha kampuni isianguke. Uamuzi huu tumeufikia kutokana na mazingira magumu yaliyotokana na:-
Madhara ya ugonjwa wa Corona uliokata mzunguko wa biashara duniani na nchini kwa ujumla.
Wadeni wetu tuliofanyanao biashara kutotulipa kwa wakati hata baada ya kuwasiliana nao mara kwa mara.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kusimamia Sheria iliyotungwa na Bunge kukusanya kodi hata kama mfanyabiashara hajalipwa na wadeni wake, hadi kufikia kuzuia akaunti za Kampuni yetu na kuchukua fedha zilizokuwamo mwezi huu.
Kwa uamuzi huu, wafanyakazi waliopunguzwa kazi kwa utaratibu maalum, wamepunguzwa mshahara kwa asilimia 80, watakuwa nyumbani, kampuni itaendelea kuwalipia Bima ya Afya (NHIF), kodi na makato ya kisheria kwa hizo asilimia 20 za mshahara watakazozipata. Kampuni itapitia uamuzi huu kila baada ya miezi sita (6) kuanzia Mei 1, 2020.
Wafanyakazi wanaobaki kazini, nao wamepunguziwa mshahara kwa asilimia 20. Kampuni italipa malimbikizo ya mishahara ya nyuma inayodaiwa na wafanyakazi mara tu itakapopata fedha.
Gazeti la JAMHURI litaendelea kuchapishwa kwa ubora ule ule katika habari za uchunguzi bila woga wala upendeleo na kama italazimu kuchukua hatua za ziada kutokana na ugumu wa uchumi unaoendelea, basi wasomaji wetu tutawajulisha muda wowote.
Kwa maslahi mapana ya uchumi endelevu wa Taifa letu, tunaishauri Serikali kwa kipindi hiki ambacho hali ya biashara ni mbaya, iweke mazingira ya kuwasaidia wafanyabiashara kwa kuwapunguzia mzigo wa kodi zinazohatarisha ustawi wa biashara nchini.
Tunawashukuru wafanyakazi wetu kwa kuelewa ugumu tulionao na kuendelea kushikamana nasi katika kipindi hiki kigumu. Tunawashukuru pia wasomaji wetu kwa kuendelea kutuamini, na siku zote tutaendelea kuiishi kaulimbiu yetu kuwa TUNAANZIA WANAPOISHIA WENGINE.