Kampuni ya Kalynda inasema niweke elfu 20 ili nipate 800 kila siku!

Hapa nimepiga swali,

kule online wanadai nisiwe mwoga nitalipwa iyo 800 kila siku. Sasa shida yangu je hiyo 20 Inaenda wapi? Kwanini nisitangaze biashara zao bila kuweka 20?

Wakuu nimekuja huku tuwekane sawa nisije lia.

Ni kweli kalynda ni njia salama jiunge nasi sasa uzuri wake unaweza anza kupata commission hata kabla ujaunganisha watu
 
Mkishaingia wa kutosha...na ikionekana hakuna wapya wanaoingia...mara paap MNAPIGWA NA KITU KIZITO
 
Kuna mtu anasumbua sana nijiunge, na mimi namtazama tu.
 
Hizi Mambo Kama akina Kalinda mi nadhani **** vigogo serikani huwa wanahusika. Maana siwezi kukurupuka kesho nikaanzisha project Kama hiyo (mfano:weka 30000, kila mwezi faida 5000)... Sitachukua round basi teyari nitakuwa ninahojiwa na watu wa TRA, Polisi nk
 
Hizi Mambo Kama akina Kalynda,DECI nk mi nadhani kuna* vigogo serikani huwa wanahusika. Maana siwezi kukurupuka kesho nikaanzisha project Kama hiyo (mfano:weka 30000, kila mwezi faida 5000)... Sitachukua round basi teyari nitakuwa ninahojiwa na watu wa TRA, Polisi nk
 
Mkishaingia wa kutosha...na ikionekana hakuna wapya wanaoingia...mara paap MNAPIGWA NA KITU KIZITO
Tayari kitu kizito,hivi watu huwa nyuzi za humu hawazipitiii? Huwa nasikitika kuona mtu yupo jamiiforums watu wanatoa elimu lakini Bado anapigwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…