1. Si haki,kwani sheria inaelekeza kuwa mtumishi akishafanya kazi kwa miezi sita au zaidi kama kibarua basi sheria inamtambua kama mwajiriwa na si kibarua,
2.sio tu si haki mtumishi kufutiwa mkataba bila kupewa sababu,bali hakuna sababu yoyote ya kumfutia mfanyakazi mkataba isipokuwa mkataba wake umekwisha au amevunja vifungu vya sheria ya ajira na mahusiano kazini au masharti ya mkataba wa ajira husika,hivho no kosa kwa mwajiri kuvunja mkataba na mwajiriwa anaweza kulipwa stahiki na fidia kama atapeleka shauri lake kwenye mabaraza ya usuluhishi na uamuzi.
3.inategemea,kwani mkataba una masharti halisi yaani express terms na mashariti butu yaani implied terms,hivyo kama mkataba unaeleza wazi kuwa baada ya kufika mwisho,pande zote zitakubaliana kama uendelee au la, kama mtumishi ataendelea bila kusaini mkataba mwingine basi assumption ni kwamba masharti yaleyale ya mkataba wa awali yanazingatiwa.
Wakati mwingine elezea vizuri tatizo lako ili upate ushauri mzuri..
Da mihi factum,dabo tibi ius----give me the fact,i will give you the law..........if u didn't know what i mean.............