Kampuni ya kitanzania na biashara ya utalii kwa nchi za egypt, tunisia, morocco and mali

Kampuni ya kitanzania na biashara ya utalii kwa nchi za egypt, tunisia, morocco and mali

C.T.U

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2011
Posts
5,074
Reaction score
3,743
wakuu habari zenu naomba msaada hapa kwenye hili..
Je mtu akitaka kuanzisha branch ya kampuni yake ya kitanzania ya utalii kwa nchi kama
egypt, morocco & tunisia inawezekana?
Je serikai zao hazina vipangamizi kwenye sekta hiyo??
Naomba kama kuna yeyote ajuaye aniambie procedures
ninatanguliza shukrani zangu ...
Tafadhali nisaidieni kwa hili
 
Mkuu kwa nini kwenye hizi nchi? je ni moja ya nchi zinazo toa wageni wengi?

- Mimi nijuavyo hata makampuni makubwa hapa Tanzania kama Leopard, Kilimanjaro safari club. Rennger safar na zingine sizani kama wana offisi katika hizo nchi.
- Mara nyingi haya makampuni huweka offisi kwenye nchi ambazo zinatoa watalii wengi sana kuja Tanzania kama vile
1. Marekani
2. Uingereza
3. Ujerumani
4 france
5. Hispania
6. Italy
7 Canada
8. Japani
Haya mataifa ndo yanatoa watalii wengi sana na hizi kampuni nyingi zina agent kwenye hizo nchi, na hata hivyo now day baada ya techinolojia kuwa kubwa booking inafanyika kupitia website za haya makampuni, so ukiwa na strong jina haina haja ya kufungua offisi huko unaweza watumia mawakala wa huko.

ILA MKUU KWA KWELI HII BIASHARA YA UTALII IMEKAMATWA SANA NA MAKAMPUNI YA WAZUNGU NA KUNA USANII MKUBWA SANA WANAUFANYA ZIDI YA MAKAMPUNI YA WAZAWA/WATANZANIA
 
nchi hizo hazina fedha. hakuna watalii wa maana. nakushauri. tafuta angalau arab gulf(saudi. uae. qatar.) na asia(malay.japan.singapore.india
 
okay thanks wadau but point yangu ni sio kuwa nataka watalii wa kutoka nchi hizo no ila ninataka kuweka ofisi ya kupeleka watalii huko...
kwa sababu hizo nchi ndizo zinazoongoza kwa watalii wengi kwenda kwa africa
idadi ya watalii wanaoenda tunisia, egypt na morrocco ni kubwa kuliko idadi ya watalii wanaokuja huku east africa
so nauliza kama inawezekana mtu ukiwa na kampuni ya utalii hapa tanzania ukafungua na ofisi huki katika hizo nchi ukawa unapeleka watalii both east africa and north africa sasa nauliza huko north africa kwa hizo nchi inawezekana kupeleka watalii??
 
Back
Top Bottom