Kiroho Safii
Member
- Aug 15, 2015
- 24
- 53
Hii ni kampuni inaitwa Orbit Group Limited (Orbit tz) inayoagiza magari kutoka nje ya nchi. Biashara hio inahusisha pia kutoa mkopo wa mpaka miaka miwili ili kukamilisha gharama ya gari.
Sasa hawa watu, kuna taarifa wanamficha mteja na wanakuja kukwambia baadae sana ambapo pengine unaweza kufikia uamuzi wa kutolichukua kabisa gari, na huku umeshatanguliza hela ya mwanzo, na ndio hapo matatizo.
Mfano, kuna ishu ilitokea (gari liliagizwa na kufika nchini) ambapo kwa makubaliano ya mwanzo, riba ya mkopo wa gari ilitakiwa iwe asilimia 3 kwa mwezi, kwa mkopo wa milioni 11, mchanganuo waliotoa ni kama huo hapo chini
Ambapo kwa mwezi ningetakiwa nilipe 650,000 tsh. Lakini, gari lilivofika nchini, wakanitaarifu kua riba imebadilika na kua asilimia 4.5 kwa mwezi, wakanipa mchanganuo mpya ambapo ningetakiwa nilipe 830,000 tsh kwa mwezi.
Ukiachilia mbali mabadiliko hayo, taarifa nyingine ni kwamba mkopo ule una gharama yake na pia gari inatakiwa ilipiwe premium, ambayo ikawa kama milioni 1.3 nyingine kutoka mfukoni.
Baada ya kufikia uamuzi wa kukataa mabadiliko haya na kuomba hela niliyolipa awali irudi, ndipo wakaanza kuzunguka. Mara wanasema mpaka gari iuzwe ndio walipe.
Na pia zaidi ya hapo. Wakaendelea kusema kwenye ile hela ya awali. Watakata gharama yao ya kuagiza gari.
Ingawa nilikubaliana na yote hayo. Bado wameendelea kuzunguka na mpaka hivi sasa kuna kesi ya madai inaendelea mahakamaini kurudisha hio hela.
Hivyo huu uzi uwe ni tahadhari kwa mtu ambae yuko kwenye hatua ya kutaka kufanya biashara na hawa jamaa. Jua kwamba sio waaminifu.
Na huu uzi sio kwamba ninaandika kuharibia biashara, hapana. Hii hapa ni screenshot ya chat na namba yao, ambayo pia wameeka kwenye ukurasa wao wa Instagram.