Laki sita unayoweka kila mwezi plus riba ukiiweka kwenye hiyo gari miezi mitatu tu inakuwa kwenye condition nzuri sana.maneno tu hayo hata kwenye kanga yapo. sa hv ukiwa na m4 cash unapata gar imenyooka kabisa.
Kuna watu si wepesi wa kukubaliana na hali, wanaforce mpaka inakuwa.Na kwanini uhangaike kununua gari kama uwezo hujafikia. Mbona sisi tunapanda daladala na mwendokasi bila shida yoyote. Siku tukipata uwezo tutanunua hayo magari.
Si mna Mkataba kama upo tumia huo mkataba kuwafungulia mashtaka ya kukiuka mkataba wakulipe pesa zako na gharama za kuendesha kesiView attachment 3056960
Hii ni kampuni inaitwa Orbit Group Limited (Orbit tz) inayoagiza magari kutoka nje ya nchi. Biashara hio inahusisha pia kutoa mkopo wa mpaka miaka miwili ili kukamilisha gharama ya gari.
Sasa hawa watu, kuna taarifa wanamficha mteja na wanakuja kukwambia baadae sana ambapo pengine unaweza kufikia uamuzi wa kutolichukua kabisa gari, na huku umeshatanguliza hela ya mwanzo, na ndio hapo matatizo.
Mfano, kuna ishu ilitokea (gari liliagizwa na kufika nchini) ambapo kwa makubaliano ya mwanzo, riba ya mkopo wa gari ilitakiwa iwe asilimia 3 kwa mwezi, kwa mkopo wa milioni 11, mchanganuo waliotoa ni kama huo hapo chini
View attachment 3056964
Ambapo kwa mwezi ningetakiwa nilipe 650,000 tsh. Lakini, gari lilivofika nchini, wakanitaarifu kua riba imebadilika na kua asilimia 4.5 kwa mwezi, wakanipa mchanganuo mpya ambapo ningetakiwa nilipe 830,000 tsh kwa mwezi.
View attachment 3056965
Ukiachilia mbali mabadiliko hayo, taarifa nyingine ni kwamba mkopo ule una gharama yake na pia gari inatakiwa ilipiwe premium, ambayo ikawa kama milioni 1.3 nyingine kutoka mfukoni.
View attachment 3056967
Baada ya kufikia uamuzi wa kukataa mabadiliko haya na kuomba hela niliyolipa awali irudi, ndipo wakaanza kuzunguka. Mara wanasema mpaka gari iuzwe ndio walipe.
Na pia zaidi ya hapo. Wakaendelea kusema kwenye ile hela ya awali. Watakata gharama yao ya kuagiza gari.
Ingawa nilikubaliana na yote hayo. Bado wameendelea kuzunguka na mpaka hivi sasa kuna kesi ya madai inaendelea mahakamaini kurudisha hio hela.
Hivyo huu uzi uwe ni tahadhari kwa mtu ambae yuko kwenye hatua ya kutaka kufanya biashara na hawa jamaa. Jua kwamba sio waaminifu.
Na huu uzi sio kwamba ninaandika kuharibia biashara, hapana. Hii hapa ni screenshot ya chat na namba yao, ambayo pia wameeka kwenye ukurasa wao wa Instagram.
View attachment 3056985
Kwa mujibu wa makubaliano ya awali alikuwa na uwezo naloPole sana mleta mada.
Lakini ndugu yangu, kwanini kuhangaika na kitu ambacho bado hujawa na uwezo nacho? kumbuka, if you cant buy it twice, you dont afford it
😂opa gangnam stylewatu wana kimuhemuhe cha magari na nikutopiga hesabu vizuri tu ila kama zimo kichwani gari sio kitu ya kukopa....
utajikuta unacheza opa gangnam style
mkuu mtu anaweza jikuta hana furaha kwenye maisha kisa madeni yasio na mbele wala nyuma.Gharama za gari= 16m
Mkopo= 11m
Inamaana ulikuwa na 5m..
Rejesho 600k+/mon==7+m/yr
Ungesubiri tu mkuu...nawewe pia utakuwa na shida mahali
Huyu anaishi kufurahisha watu...mkuu mtu anaweza jikuta hana furaha kwenye maisha kisa madeni yasio na mbele wala nyuma.
hizo 7m angeweza kuziwekeza kwenye jambo la maana kabisa alafu gari yenyewe sio ya biashara....
But the slogan doesn't work in bongolandPole sana mleta mada.
Lakini ndugu yangu, kwanini kuhangaika na kitu ambacho bado hujawa na uwezo nacho? kumbuka, if you cant buy it twice, you dont afford it
Mkuu hao peleka mahakamani,na kesi iwe na fidia ya usumbufu waliosababisha!Niliusoma mkataba vizuri sana na haya yote hayakusemwa. Ni kwamba hawa watu wamekuja kubadilika kwa maneno makavu bila kufuata mkataba waliouandika wenyewe. Na ingawa wanajua kua wamekosea na wanatakiwa kurudisha hela, ambapo hata mwanasheria wao ambae ndie ameweka mhuru kwenye mkataba amewashauri hilo, wanazunguka zunguka. Ninavosema kua ni matapeli, ni matapeli kweli!
Kwa mujibu wa makubaliano ya awali alikuwa na uwezo nalo
But the slogan doesn't work in bongoland
Daah ***** nimecheka....Ni sawa tu na kampuni ya mikopo ya Jipimiekash hawa wanakupa mkopo kwa makubaliano utarudisha tarehe 1 mwezi ujao na umekopa tarehe 26 lakini ikifika tarehe 28 anapiga simu mwanamke anataka ulipe pesa hiyo siku hiyo kabla jua halijazama anasema hiyo tarehe 1 ni makubaliano ulifanya na kampuni ila yeye anataka tarehe 28
Unajizuia tu kutukana
Sure mkuuSasa imagine mtu ananunua gari kwa kuunga unga ikifika tarehe 15 anapaki sababu hela ya zutu imekata. Gari ikihitaji major repair ya kuanzia 1 m mtu anaanza kupata depression. Siku tukijifunza kuishi within our means, mambo yatakua matamu.