Kibukuasili
JF-Expert Member
- May 15, 2010
- 1,053
- 615
Nafikiria kuanzisha kampuni ya kupandisha wageni mlima kilimanjaro. Kwa sasa ninachojua ni kwamba.
Mwenye uzoefu na hii kitu tafadhali anipatie maelezo ya ziada au anisahihishe kuhusu hayo niliyoyataja hapo juu.
- Lazima uwe na kampuni iliyosajiliwa BRELA na TRA.
- Sio lazima kuwa na gari. Magari ya kuwachukua airport kwenda hotelini na kwenye geti la kuanzia/kumalizia unaweza kukodisha.
- Nguo za kupanda mlimani wengine wanakuja nazo na za kukodi zipo pia.
- Wabeba mizigo, wapishi na waongozaji ni watu wa kulipwa kutwa. Viongozi wao ni vizuri ukawaajiri.
- Makampuni ni mengi wateja wachache, lakini juhudi yako ndio utafanikiwa.
Mwenye uzoefu na hii kitu tafadhali anipatie maelezo ya ziada au anisahihishe kuhusu hayo niliyoyataja hapo juu.