BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Huku kwetu mtaa ya Mbezi ya Chini (Mbezi Chini) kuna changamoto moja ambayo imekuwa kero kwa watu wengi kuhusu uzoaji taka.
Iko hivi, mamlaka za Serikali za Mtaa za mitaa ya Mbezi Chini, Afrikana na sehemu nyingine ambazo bado sijajua zimekuwa zikitoza kiasi cha shilingi 3,000 hadi 5,000 kwa kila nyumba kwa ajili ya taka za nyumbani.
Yaani kila nyumba inatoa kiasi hicho cha fedha, lakini kuna kampuni ambayo imepewa tenda ya kukusanya taka kwenye nyumba mbalimbali yenyewe imekuwa ikiongeza cha juu na kutoza hadi shilingi 15,000 kwa nyumba.
Inavyoonekana wanachagua baadhi ya nyumba wakiona mambo safi, basi wanaongeza bei na sio ile buku tatu kama inavyotozwa za Serikali za Mtaa.
Naomba mamlaka ziangalie kinachoendelea kwani hii hali inatuumiza, kwa jinsi gharama za maisha zilivyo juu, tuna mambo mengi ya kufanya na yanayotupa stress, hawa wazoa taka nao wanakuja kutongezea stress, watatupasua kichwa
Changamoto nyingine ni hii Kampuni iliyopewa tenday a kukusanya taka, kwanza ukiwauliza kampuni yao inaitwaje wao wanakwambia tu wewe toa hela na kudai wao ndio wamekabidhia jukumu hilo.
Ukiuliza Serikali za Mtaa nao inavyoonekana kuna watu wamepiga cha juu kwa kuwa hawatoi majibu ya kueleweka kuhusu kampuni walizozipa tenda.