Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo Ofisini kwake Mei 15, 2023 Mtumba jijini Dodoma na wawakilishi wa Kampuni za Limonta na Reen Line za nchini Italia kuhusu kujenga na kuboresha miundombinu ya Michezo nchini.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nicholas Mkapa, MKurugenzi wa Sera na Mipango Abel Shirima, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Addo Komba pamoja na baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo.