DOKEZO Kampuni ya Macrobuluba Investment imeshindwa kutekeleza wajibu wa ukusanyaji taka mtaa wa Kisewe, Temeke

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

wekandani

New Member
Joined
Jun 1, 2026
Posts
1
Reaction score
0
Sisi wakazi wa Mtaa wa Kisewe, Wilaya ya Temeke, tunapenda kuwasilisha malalamiko yetu kuhusu utendaji usioridhisha wa kampuni ya MACROBULUBA INVESTMENTS COMPANY LTD ambayo imepewa jukumu la ukusanyaji wa taka katika eneo letu.

Kwa muda mrefu sasa, kampuni hiyo imekuwa ikishindwa kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi, jambo ambalo limesababisha kero kubwa kwa wananchi na kuhatarisha afya pamoja na mazingira ya wakazi wa mtaa wetu.

Changamoto tunazokabiliana nazo ni pamoja na:
  1. Ukusanyaji hafifu wa taka – Kampuni hukusanya taka mara moja tu kwa mwezi, hali inayosababisha taka kujaa katika makazi ya wananchi na maeneo ya umma kwa muda mrefu.
  2. Kutotoa risiti kwa kutumia mashine za POS – Licha ya kukusanya fedha kutoka kwa wananchi, kampuni haijatoa risiti za kielektroniki kupitia mashine za POS kama inavyotakiwa, jambo linalozua maswali kuhusu uwazi na usimamizi wa mapato yanayokusanywa.
  3. Matumizi ya usafiri usiofaa wa kubebea taka – Kampuni imekuwa ikikusanya taka kwa kutumia guta(Toyo) ambayo hayajaandaliwa mahsusi kwa kazi ya ukusanyaji taka, hali inayochangia uchafuzi wa mazingira na kutokidhi viwango vinavyotarajiwa vya usafi wa mazingira.
  4. Vitisho na unyanyasaji wa wananchi – Baadhi ya wakusanyaji mapato wa kampuni wamekuwa wakitumia lugha za vitisho, matusi na unyanyasaji wa kihisia dhidi ya wananchi wanaouliza kuhusu malipo au huduma wanazopaswa kupata.
Kutokana na hali hiyo, tunaomba Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ifanye uchunguzi wa haraka kuhusu utendaji wa kampuni hii na kuchukua hatua stahiki ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya ukusanyaji taka kwa mujibu wa masharti ya mkataba na sheria za usafi wa mazingira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…