DOKEZO Kampuni ya Mafuta ya Lake Oil zamani sasa Lake Energies, inafukuza wafanyakazi wake kiholela bila kufuata sheria za kazi

DOKEZO Kampuni ya Mafuta ya Lake Oil zamani sasa Lake Energies, inafukuza wafanyakazi wake kiholela bila kufuata sheria za kazi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kampuni ya Mafuta ya Lake Oil zamani sasa Lake Energies, inafukuza wafanyakazi wake kiholela bila kufuata sheria za kazi.

Mtumishi anaondolewa kazini bila kupewa barua yoyote ile wala kulipwa Stahiki zake za msingi na hata mishahara ya mwezi husika aliokuwepo kazini.

Ndani ya mwaka huu wamefukuza zaidi ya wafanyakazi kumi na tatu bila sababu za msingi, ni vile tu kuna viongozi wa ngazi za juu wanatengeneza safu zao za wizi.

Vijana wanarudi mtaani wanateseka, kwani hawawezi kuajiriwa sehemu zingine kwani hawana barua za kuachishwa kazi wala certificate of service.
Hili limekuwa kawaida kwao lakini wanaoumia ni vijana masikini wa kitanzania.

Hili lipaziwe sauti
 
Kapambane kwingine,,,,pengine hapo sio rizk yako ilipo! Mlango mmoja ukifungwa , mwingine hufunguliwa
 
Kufanya kazi kwa waarabu,wachina na wahindi inabidi uwe na roho ngumu na mtu wa kujipendekeza sana kwa maboss.
We anagalia tu Manara anavyojipendekeza kwa GSM.
 
Back
Top Bottom