Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
KAMPUNI ya Mantra Tanzania inayosimamia mradi wa uchimbaji urani eneo la mto Mkuju wilayani Namtumbo Mkoa wa Ruvuma, imesisitiza kushirikiana na jamii inayozunguka eneo la mradi kwa
kusaidia shughuli mbalimbali, zikiwemo za kijamii. Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Asa Mwaipopo alisema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari.Alisema kampuni
imeweka kipaumbele cha kusaidia jamii katika masuala mbalimbali, ikiwemo utoaji ajira kwa Watanzania wengi. Mwaipopo alisema lengo la kampuni ni kuhakikisha inaijengea jamii uwezo,
ukiwemo wa biashara ili ipige hatua za kimaendeleo.Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzania, Khadija Palangyo alisema pamoja na kuunga mkono shughuli za kijamii na
kiuchumi, kampuni imeweka mkakati wa kuelimisha na kufahamisha jamii shughuli zake iuelewe kwa ufasaha.Alisema waandishi wa habari ni wadau muhimu, ambao kampuni inahitaji wafahamu
mambo mbalimbali sanjari na kutembelea mradi, kwa lengo la kuhabarisha umma.Mradi wa Urani wa Mto Mkuju, kulingana na utafiti wa kina wa madini ya urani, uliofanywa katika eneo la mradi,
uligundua mashapo yanayoweza kuchimbwa kibiashara. Taarifa zinaonesha zipo tani milioni 175.8 za mashapo ya urani zilizogunduliwa. Kiasi hicho ni sawa na kilo milioni 52.5 za urani .Kulingana na
mashapo hayo, uhai wa mgodi kwa sasa ni miaka 12. Mradi huo wa Mto Mkuju unamilikiwa na Kampuni ya Mantra Tanzania Limited, ambayo ni Kampuni tanzu ya URMZ ya Urusi. Mradi huu uko
ndani ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Selous.Pia eneo hilo ni Sehemu ya Urithi wa Dunia. Hata hivyo Julai mwaka juzi, Tume inayohusika na masuala ya urithi wa dunia, iliyoko chini ya Unesco
ilitoa idhini ya kuondoa eneo la Mradi wa Mto Mkuju kwenye eneo la Urithi wa Dunia ili uchimbaji wa urani uweze kufanyika.Hata hivyo, eneo hilo litaendelea kuwa ndani ya eneo la Hifadhi ya
Wanyamapori la Selous. Kutokana na hatua hiyo, uchambuzi wa masuala ya mazingira ulikamilika Oktoba, 2012 ambapo Hati ya Mazingira ilitolewa na Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
nchini (NEMC).Baada ya hatua hizo kukamilika, Wizara ya Nishati na Madini ilitoa leseni ya uchimbaji madini ya urani Aprili mwaka jana. Leseni hiyo inaruhusu uchimbaji kufanyika katika
mradi huo.Majadiliano kuhusu mkataba wa kuendeleza uchimbaji madini kuhusu mradi yanaendelea. Uchimbaji wa madini ya urani katika mradi wa Mto Mkuju, utafanyika hadi hatua ya
yellow cake.Baada ya hapo urani hiyo itasafirishwa kwenda nje ya nchi katika maeneo ambayo urutubishaji wa madini hayo kwa matumizi mbalimbali, kama vile kuzalisha umeme, kutengeneza vifaa vinavyotumika kwenye sekta za afya, kilimo, ujenzi na mifugo.http://www.touch.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/20972-kampuni-ya-mantra-kushirikiana-na-jamii