Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet yawapa shavu la udhamini michuano ya Ruvuma Vijana Cup

BongeMwepesi

Senior Member
Joined
Aug 13, 2013
Posts
125
Reaction score
83
Akizungumza leo Msemaji wa M-Bet Tanzania amesema wamefikia hatua hiyo ya kudhamini ligi hiyo ya Ruvuma Vijana Cup Ikiwa ni muendelezo wao wa kusapoti kuibuliwa kwa vipaji vya vijana wa Kitanzania na wataendelea kufanya hivi kwenye tournaments mbalimbali zinazoendelea nchini. Lakini pia ni muendelezo wa kuunga mkono michezo Tanzania ndiyo maana walishadhamini pia timu ya KMC ambayo inashiriki ligi kuu ya Tanzania.

Akizungumza kwa niaba ya waratibu wa Ruvuma Vijana Cup Ndg. Raymund Mhenga amesema anawashukuru sana Kampuni ya Michezo ya kubashiri ya M-Bet kwa kukubali kuwa wadhamini rasmi wa michuano hiyo na kwamba kupitia udhamini huo basi utasaidia sana kuibuliwa kwa vipaji vya vijana wengi mkoani Ruvuma.

Kampuni ya Michezo ya kubahatisha ya M-Bet wametoa vifaa vyote vya michezo kwa timu shiriki ambazo zitaingia hatua ya 16 bora na mambo kadha wa kadha yanayohusiana na Ruvuma Vijana Cup.

Mhenga alisema kwa niaba ya vijana wa mkoa wa Ruvuma anakaribisha pia wadau mbalimbali kuja kuwekeza kwenye michezo mkoani Ruvuma kwani asili ya watu wa mkoa wa Ruvuma ni wanamichezo na pia ni watu wenye vipaji vya sanaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…