Kwa msiofahamu tumbaku hununuliwa na makampuni tofauti. Makampunj yaliyopewa leseni ya kununua tumbaku mkoani Tabora ni pamoja na Voedsel, Alliance One, TLTC, GTI, Mkwawa na mengine nimeyasahau.
Katika makampuni yote haya kampuni iliyopewa zabuni kubwa zaidi ni Mkwawa Leaf kwa madai kuwa ni kampuni ya wazawa. Na ilipigiwa promo sana na vyombo vya habari pamoja na serikali.
www.jamiiforums.com
Masoko ya ununuzi wa tumbaku mwaka huu yalifunguliwa mwezi April, na makampuni yalipewa sharti la kuwalipa wakulima fedha zao ndani ya wiki mbili tu. Makampuni karibu yote yametekeleza sharti hilo, na hivi ninavyoandika dokezo hili vyama vyote vya ushirika wa wakulima vilivyouza tumbaku yao katika makampuni ya kigeni wamelipwa fedha zao.
Lakini wakulima waliouza tumbaku yao kenye kampuni ya Mkwawa Leaf tangu mwezi April mpaka leo wanapigwa kalenda.
Kiburi cha kamapuni hii kinatoka wapi?
Za ndani kabisa zinasema kampuni ya Mkwawa Leaf imeundwa na vigogo wa serikali pamoja na wafanyabiashara wakubwa ikiwa ni pamoja na waziri Bashe. Nani atawagusa hawa? Wakubwa waliopaswa kuwasaidia wakulima nao wanashiriki dhulma.
Bashe akiwa mbele ya kamera anaongea mpaka povu linamtoka akiigiza kuwatetea na kuwapigania wakulima. Lakini kwenye suala la dhulma inayofanywa na kampuni ya Mkwawa Leaf hasemi chochote kwasababu naye ni miongoni mwa wahusika katika dhulma hii.
Katika makampuni yote haya kampuni iliyopewa zabuni kubwa zaidi ni Mkwawa Leaf kwa madai kuwa ni kampuni ya wazawa. Na ilipigiwa promo sana na vyombo vya habari pamoja na serikali.
Mkwawa Leaf yawakomboa Wakulima wa Tumbaku
MKWAWA LEAF YAWAKOMBOA WAKULIMA WA TUMBAKU Kampuni ya Mkwawa Leaf Tobacco imeshusha neema kwa Wakulima wa Tumbaku nchini, Kampuni hiyo inatojishughulisha na Ununuzi wa Tumbaku nchini imeungana na Sera ya Serikali ya Kilimo katika Kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasan kwa kuhakikisha...