Kampuni ya Samsung kumtangaza msanii Vanessa Mdee kuwa balozi wa kampuni hiyo

lyzbeth

Member
Joined
Mar 6, 2014
Posts
40
Reaction score
8
Kampuni ya kielektroniki ya Samsung kwa mara ya kwanza imehusisha kampuni hiyo na msanii wa muziki kutoka nchini Tanzania. Leo hii, Kampuni namba moja duniani inayoongoza kwa technolojia ya hali ya juu, Samsung wanayo furaha kumtangaza balozi wao mpya mwanamziki nyota, na mtangazaji wa Televisheni na radio Vanessa Mdee.

Katika mkutano na wanahabari ulilofanyika hoteli, ya Hyatt Regency, iliyoko mjini Dar es Salaam iliohusisha kusaini kwa mkataba baina ya Vannesa Mdee na uongozi wa kampuni ya Samsung ni ishara tosha ya makubaliano rasmi kati ya Kampuni ya Samsung na msanii huyo. Kitendo hicho kilihashiria mwanzo wa kazi mpya kwa Vanessa Mdee kama mwakilishi wa kampuni ya Samsung nchini Tanzania.

Akiwa kama balozi wa kampuni ya Samsung, Vanessa atakuwa kiungo muhimu katika muonekano na uzinduzi wa bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kielektroniki ya Samsung, Mheshimiwa Mike Seo alisema kuwa, "kwa kutambua ongezeko la uhitaji wa simu za kisasa kwa soko la kati nchini Tanzania ni bora kuwasiliana na wateja wetu kupitia mtu ambaye amebeba sifa zinazoendana na vifaa vyetu na soko letu.

Anaongeza kuwa "Tunafuraha sana kutangaza ushirikiano wetu na Vanessa Mdee akiwa kama Balozi wetu mpya nchini Tanzania. Akiwa kama mwanamziki nyota na mchangiaji chanya kwa wananchi wa Tanzania. Vanessa anawakilishi vijana wa kisasa wa Tanzania na ni mtu ambaye kampuni ya Samsung inaweza kufanya naye kazi hivyo basi tuna furaha kubwa kuwa na mtu kama huyu kuwakilisha bidhaa zetu. "

Vanessa Mdee ambaye aliongozana na menejimenti yake kwenye mkutano huo, alielezea juu ya furaha yake kwa kuwa sehemu ya kampuni ya Samsung, alisema "Samsung ni kampuni kubwa na yenye hadhi ya juu, ni heshima kubwa sana kwangu kuwa balozi wa kampuni hii inayoongoza kwa kutengeneza vifaa vya kielektroniki ulimwengu, huu ni mwanzo tu wa jinsi mwaka 2015 utakavokuwa wa mafanikio kati yangu na kampuni ya Samsung. Binafsi, natumaini juu ya kazi hii na nasubiri kwa hamu siku nitakayoanza kazi rasmi. "
 
bora wangempa jide tu aliyesota miaka mingi na kuitambulisha nchi kimataifa huyo mbuzi kaja juzi tu apa ata hajapata msoto wanampa ubalozi

uyu sista simuelewi elewi kiukweli kama anaviconnection flani kuhusu ma deal anayopiga labda kisa utangazaji wa Mtv
 
hongera vanesa, piga kazi mtoto na uwe na malengo baadae usije bwia unga mama, angalia waliokutangulia ujifunze kutoka kwao. kila la heri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…