herikipaji
JF-Expert Member
- Aug 23, 2016
- 1,198
- 1,369
Unamaanisha nini
Mimi bwana nakupongeza 20%, iliyobaki naweka akiba ya maneno. Hii mibasi yenu Made in Hu Ha siiamini hata kidogo. Nimepanda Happy Nation Semi Luxury kutoka Dar naenda Moshi, tumefika Hedaru nasikia joto lenye makero. Kumuuliza konda kisa cha kuzima kiyoyozi, naambiwa imezimwa kwa kuwa ikiwashwa engine inakosa nguvu. Nikauliza kile kinyongeza cha nauli ya semi luxury kitarudi mfukoni mwangu...nikaambiwa mimi mtata.Mama kwa hakika serikali ya Tanzania haikukosea kuipa cheti cha ushindi kwa mabus ya Tahmeed. Sasa Tahmeed wamezidi kudhihirisha kuwa wataendelea kuwa vinara kwa vipindi vyote na kukosa mpinzani kwa kuleta mabus mapya aina ya zhongtong ambayo ndani yana muonekano kama ndege za boeing ,kwani hadi sasa ndio mabus pekee yenye siti za 2 by 1 mwanzo hadi mwisho wa bus. niliwahi kuwaahidi miezi minne nyuma kuwa watanzania wajiandae kwa ugeni huu mzito.
View attachment 465297 View attachment 465298 View attachment 465299
Tahmeed coach
your comfort
is our concern
Labda cheti cha ushirikiCheti cha ushindi? Ushindi wa nini? Hebu kiweke hapa hicho cheti.
Ila hongera sana kwa mabus mazuri
exactlyHongera haya ndo mambo tunataka kuyaona, ushindani kwa ubora na huduma.... Wengine watajifunza kwenu na watakuja na za airbus na zingine ....
Nani wewe:mkuu mbona unatutukana sisi waha
Acha mbwembwe nilishakupa wazo kwanini msianzishe route za Dar es salaam via rombo nairobi au haiwezekani?Mama kwa hakika serikali ya Tanzania haikukosea kuipa cheti cha ushindi kwa mabus ya Tahmeed. Sasa Tahmeed wamezidi kudhihirisha kuwa wataendelea kuwa vinara kwa vipindi vyote na kukosa mpinzani kwa kuleta mabus mapya aina ya zhongtong ambayo ndani yana muonekano kama ndege za boeing ,kwani hadi sasa ndio mabus pekee yenye siti za 2 by 1 mwanzo hadi mwisho wa bus. niliwahi kuwaahidi miezi minne nyuma kuwa watanzania wajiandae kwa ugeni huu mzito.
View attachment 465297 View attachment 465298 View attachment 465299
Tahmeed coach
your comfort
is our concern
Utakua hufahamu historia ya Tanga na Mombasa, wenye mabasi hayo ni wakazi/wenyeji wa Tanga walienda Mombasa kufuata biashara baada ya biashara na viwanda kuanguka/kufungwa Tanga miaka ya 1980, bado familia zao zipo Tanga na ndio maana baadhi ya mabasi yao yana plate number za Kenya na mengine za Tanzania, kifupi kuna mwingiliano mkubwa kati ya watu wa Tanga na MombasaTahmeed is a Kenyan company sielewi kwa nini wanapewa ruhusa kuserve domestic routes. Serikali amkeni!
Nipo hapa mkuu, naona Tahmeed kila iitwapo leo anafanya yale ambayo wengi wetu tunahitaji.mkuu chakii pita hapa
Mimi bwana nakupongeza 20%, iliyobaki naweka akiba ya maneno. Hii mibasi yenu Made in Hu Ha siiamini hata kidogo. Nimepanda Happy Nation Semi Luxury kutoka Dar naenda Moshi, tumefika Hedaru nasikia joto lenye makero. Kumuuliza konda kisa cha kuzima kiyoyozi, naambiwa imezimwa kwa kuwa ikiwashwa engine inakosa nguvu. Nikauliza kile kinyongeza cha nauli ya semi luxury kitarudi mfukoni mwangu...nikaambiwa mimi mtata.
Safiri leo njia ndefu kama Dar Mwanza, angalia break down za Hu Ha, zote gari mpya mpya lakini majanga kibao. Mimi niwaombe sana wafanya biashara nyinyi, hizo video zenu mtembee na jenereta. Linapokufa jumba hilo basi angalau fidio iendelee kuwaburudisha mkisubiri spea kutoka Dar.
Nitajitahidi nipande moja yangali mabichi ili nilinganishe na Bombadier. Msisahau kugawa maji na shalbati twende tukiburudika. Ila tafadhali msigawe Juice za Azam, kuna watu tuna mgomo wa bidhaa za Azam tangu matokeo ya mechi ya juzi...kila la kheri!
Sasa ww hyo milango huko hewani unataka ijifungue ili iweje sasa au unataka ushuke kuchimba dawa mawinguni?Mkulu angenunua kama haya kuliko bombardier zinazogoma kuwaka na kufunguka milango ikiwa hewani
Hahahaaaa kama kakujambisha vile[emoji36][emoji36][emoji36][emoji36]kama vip mpe makavuUnatangaza biashara au siasa[emoji57]
Musoma abiria hulala humohumo so watayachafuatupelekeeni Musoma basi moja basi
Una balaa weewee..Naombeni kazi falcon mombasa
Hahaha noma kweliHongera zao.
Wengine wanalia hela hakuna.
Sijui waliambiwa kuna soko linalogawa hela za bure!
Hu Ha sio watu wale. Lakini wafanyabiashara wanayapenda sijui ni bei au nini. Mimi kati ya 2004 - 2007 nilikuwa napanda Arusha mara kwa mara, basi langu lilikuwa Royal Coach, Scania Marcopolo zile Andare za Brazil. Nimeshangaa 2014 kulikuta basi hilo Mtwara. Nimepanda bado linakamua sawa sawa na sisikii makelele ya vioo vya madirisha japo Nyamwage bado ina rough road.Mkuu inaweza kuwa kweli kwa sababu ni jana tu nimetoka Tanga na moja ya magari mapya (jina kapuni) ya huko huko Hu Ha, nalo likaharibika . Nadhani ilikua ni timing belt, kwani niliiona imekatika. kwanza lilianza kwenda taratibu na AC ikazimwa baada tu ya kumaliza mlima wa Wami na kufika minzani likapaki kwa matengenezo. Wengine tulikubali kupanda basi la kampuni nyingine ya Tanga kukamilisha safari yetu mapema. Waliogoma sijui waliondoka vipi na muda gani waliondoka!
kwa nn wasiweke one by one ndo tujue wababe nafasi inayobak ya kukunjua kitanda ama kunyooshea miguu...kila mtu aangalie anachokipenda kwenye tv yake ..Ni mazuri ila siti za kati watakuwa wanasumbua sana watu wa dirishani
Duh, na hilo nalo ni jina la basi? majina mengine hata ukidhulumiwa kwenye basi utaogopa kwenda kushitaki.Tangazo limekosa logo tu.
Kuna RATCO, KIMBINYIKO, TABORA EXPRESS, SHABIBY, BUTI LA ZUNGU wote hao wanazo