Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Kampuni ya Orano ya nchini Ufaransa imepoteza udhibiti wa mgodi wa Uranium wa Airlit wa nchini Niger uliokuwa ukiendeshwa na Kampuni tanzu ya Orano iitwayo Somair. Orano ambayo ni kampuni inayomilikiwa na serikali ya Ufaransa, ilikuwa inamiliki asilimia 63.4 ya hisa za Somair huku serikali ya Niger ikimiliki asilimia zilizobaki.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Orano mnamo tarehe 5 Disemba 2024, kampuni hiyo ilisema kwamba imepoteza udhibiti wa mgodi huo na kwamba serikali ya kijeshi ya Niger kwa sasa ndiyo inadhibiti shughuli zote za uendeshaji wa mgodi .
Hili ni pigo lingine kwa kampuni ya Orano ambayo mwezi Juni mwaka huu serikali ya kijeshi ya Niger iliifutia leseni ya kuendesha mgodi mwingine wa Uranium uitwao Imouraren. Mgodi huo ambao ni miongoni mwa migodi mikubwa zaidi ya Uranium duniani, unakadiriwa kuwa na takribani tani laki mbili za Uranium ambazo hazijaanza kuchimbwa bado.
Tangu mapinduzi ya Niger ya Julai 2023 yaliyomtoa madarakani Rais kipenzi cha Ufaransa Bw Mohammed Bazoum, kampuni ya Orano imepitia wakati mgumu hali iliyoisababishia faida yake kupungua kwa mamilioni ya Euro. Pia Umoja wa Ulaya ambao robo ya Uranium yake inayotumika kuzalisha Umeme ilikuwa ikitoka nchini Niger, umelazimika kununua Uranium kutoka nchini Urusi kinyume na mpango wake wa kuacha kununua raslimali za Urusi ili kuidhoofisha kiuchumi serikali ya Vladimir Putin.
Nchi ya Niger ilikuwa muhimu sana kwa uchumi wa Ufaransa kutokana na kuwa tangu mwaka 1971 kampuni ya Orano ilichimba Uranium ya Niger na kuitumia kuzalisha umeme uliokuwa unatumika nchini Ufaransa na mwingine ulikuwa ukiuzwa nchi nyingine za Ulaya. Orano ilikuwa ikitengeneza mabilioni ya Dollar kwa kutumia Uranium ya Niger huku nchi ya Niger ikiwa haiambulii kitu chochote na kusalia kuwa nchi maskini zaidi duniani. Kabla ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2023 migodi yote ya Uranium iliyopo nchini Niger ilikuwa chini ya udhibiti wa Orano.
Serikali ya kijeshi ya Niger inayoongozwa na Brigedia Jenerali Abdul Rahman Tchiani imeamua kuiondoa Orano nchini Niger na kuwatafuta wawekezaji wapya ingawa hadi sasa hakuna muwekezaji mwingine aliyethibitishwa kuchukua nafasi ya Orano. Pia serikali hiyo ya kijeshi imewekeza nguvu nyingi zaidi kwenye sekta ya mafuta kwa kuanza kuuza mafuta ghafi kwenda nchi nyingine na kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta ( Refinery) na kiwanda cha Plastki( Petrochemical Complex) ambavyo vyote vitatumia raslimali ya mafuta ghafi yaliyopo nchini humo.
Uuzwaji wa mafuta nje ya nchi ulioanza mwaka 2024 umeifanya nchi ya Niger kuwa na uchumi unaokuwa zaidi barani Afrika na wa tatú kwa dunia kwa chumi zinazokua zaidi kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la fedha la kimataifa IMF.
Chanzo/ Source: Yahoo Finance , Orano Website.