Jambo wandugu, nina kampuni ya ujenza Class VII. Imesajiliwa na ina leseni zote lakini kwa bahati mbaya haipati kazi kwa sababu mbalimbali. Natafuta mtu ambaye ana uwezo wa kupata kazi lakini hana kampuni wala mtaji akajiunga nasi ili tutafute kazi kwa pamoja. Awe na uwezo wa kusimamia kazi zitakazopatikana. Kampuni ninayo na mtaji upo lakini kazi sina. Tutazungumza namna gani ya kugawana mapato yatayopatikana. Kama una interest tafadhali ni-pm.
Mkuu.WEKA MAELEZO YA KUTOSHA ILI WATU WAJUE NA WAKUPE USHAURI, KWA NINI UKOSE KAZI ZA KUFANYA?!, AU KUNA TATIZO KATIKA USIMAMIZI WA KAMPUNI YAKO?.SASA UTAWEZA VIPI KUPATA MSHIRIKA PASIPO KUWA MUWAZI JUU YA MATATIZO YANOISIBU KAMPUNI YAKO?.
Nyie ndio mnaoangusha majumba kwa kujenga bila viwango? Teh teh teh ... .... Unataka utajiri kwenye fani ambayo hata huielewi. Tangaza kazi na uwalipe professionals kiwango kinachotakiwa na wao kwa kutumia usomi wao na qualifications zao watapata kazi. Kama kweli mpunga unao kama unavyosema tangaza kumtafuta managing director aliyebobea na weka sifa zake wako wengi tu siku hizi hapa bongo. Angalia wasikuletee vyeti vya kugushi. Good luck.
Fani ya utajiri ni ipi? Nadhani unatakiwa kurudia kusoma nilichoandika. Isingesajiliwa bila kufuata taratibu zote.
Mitiki huwa nasikia ni dili sana.....lakini ulichokosea mkuu makola ni kuchomekea mada kwenye thread ya Jamaa wa kampuni ya ujenzi.waungwana nina mitiki 150 ina umri wa miaka 20. Nipeni bei tangaza dau. Miti ipo maeneo ya tanga handenoi