Kampuni ya Vodacom Tanzania imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za ubunifu wa aina mbalimbali unaofanywa nchini Tanzania

Kampuni ya Vodacom Tanzania imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za ubunifu wa aina mbalimbali unaofanywa nchini Tanzania

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Vodacom yaahidi kuwekeza zaidi katika maswala ya uvumbuzi

Kampuni ya Vodacom Tanzania imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za ubunifu wa aina mbalimbali unaofanywa nchini Tanzania.

Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Phillipe Besiimire Jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya miaka 10 tangu kampuni ya Vodacom ianze kutoa ushirikiano wake katika wiki ya ubinifu inayofanyika kila mwaka.

"Kuna mwanga wa mafanikio makubwa kupitia ubunifu katika siku zijazo; tunaamini katika nguvu ya sayansi na teknolojia;wote tunajua kwamba uvumbuzi unaweza kutoa mchango mkubwa katika kukuza kiuchumi na mswala mengine ya kijamii kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, afya na changamoto ya ukosefu wa ajira," alisema.

Aidha alibainisha kuwa Vodacom Tanzania inajivunia kuwa sehemu ya familia ya Wiki ya Ubunifu nchini Tanzania katika safari yake (wiki ya ubunifu) ya miaka 10 ambayo imewanufaisha vijana wengi wenye vipawa vya ubunifu kuboresha maisha yao.

Alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).

Naye Mkurugenzi wa Usimamizi wa Ujuzi katika Tume ya Sayansi na Teknolojia, Samson Mwela, aliipongeza Vodacom Tanzania kwa kuwa miongoni mwa wadau wakubwa wa ubunifu hapa nchini.

"Mmejidhihirisha kwa vitendo kwa kuunga mkono wiki ya uvumbuzi kwa miaka 10 sasa; swala hili ni la kutia moyo lnapokuja swala la kukuza ubunifu hapa nchini; tunatoa wito kwa mashirika mengine kuiga mfano huu, kwani kuna vipaji vingi ambavyo vinahitaji kuibuliwa”, alisema.

Alisema serikali inapenda kufanya kazi na taasisi kama Vodacom Tanzania katika kuhakikisha ubunifu unapewa kipaumbele kwa kutokana na ukweli kwamba ubunifu ni chachu ya maendeleo.

Naye Meneja Programu wa taasisi ya Funguo, Joseph Manirakiza, ambaye shirika lake linaratibu Wiki ya Ubunifu kwa ushirikiano na tume ya sayansi na teknolojia (Costech), alisema Vodacom imekuwa mshirika mkuu wa Wiki ya Ubunifu na imekuwa thabiti kwa miaka 10 iliyopita.

"Hii ilikuwa kampuni ya kwanza kudhamini Wiki ya Ubunifu tulipoanza maadhimisho haya miaka 10 iliyopita na imekuwa nasi kwa muda wote huo," alisema.

Taasisi nyingine ambazo zimekuwa na jukumu kubwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya (EU), FCDO, shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP) ambao wameendelea kufanya taasisi ya Funguo kuwa imara na smbamba na washirika wengine ambao wamekuwa wakiunga mkono wiki ya uvumbuzi ambao ni pamoja na UNICEF, shirika la umoja wa mataifa la wanawake (UNWOMEN), ENABEL na VODACOM.
 
Back
Top Bottom