Kuna taarifa kutoka katika chanzo cha uhakika kwamba kampuni la Alpha ambazo zinamilikiwa na familia ya Edward Lowassa ambazo zinatengeneza mabilioni ya shilingi katika mitandao yake ya kibiashara, zimekuwa zikikwepa kodi mbalimbali ambazo zinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara wote, kama vile kodi ya mapato, import duties kwa bidhaa wanazoagiza pamoja na kufanya mawasilisho ya VAT wanayokusanya kutoka kwa wateja wao.
Taarifa zinasema kwamba mchezo huu mchafu ambao hauzingatii hata sheria na mamlaka zinazotakiwa kutoa misamaha hiyo, zinafanyika kwa ushirikiano na vigogo wa TRA ambao wako kwenye pay roll ya wamiliki wa kampuni hizo. Kutokana na ukubwa wa biashara za Alpha na ukubwa wa mapato yao, mapato wanayokwepa yanakadiriwa kuwa ni kwenye mabilioni ya shilingi kila mwezi na yangeweza kuinua pakubwa katika pato la taifa na kwa kufanya hivyo, nchi hii inazidi kudidimizwa na wale wale ambao leo wanataka kupewa dhamana za uongozi katika taifa hili.
Wakati suala hili linaweza kuonekana ni la kawaida hapa nchini kwetu kutokana na kukosekana kwa nia thabiti ya kudhibiti vitendo vya kudhibiti mapato na rasilimali za taifa, katika nchi zilizoendelea kama Marekani mmiliki wa biashara hizi asingethubutu hata kuomba ujumbe wa nyumba kumi akakubaliwa. Huu ni wakati wa watanzania kuamka na kuelewa kwamba tunaposema kwamba Lowassa si mtu safi na aisyestahili kupewa heshima anayopewa na baadhi ya wapambe ambao wameleweshwa na fedha haramu! Umefika pia wakati wa kuifagia TRA maana madudu yao yanazidi kuwawamba watanzania katika msalaba mkali sana wa maisha!
Yote yaliyosemwa kuhusu waziri mkuu 'mstaafu' yanatosha sasa.
Kuna mambo mawili ya kufanya hapa.
1.Afunguliwe mashtaka sheria ichukue mkondo wake.
2.Tuendelee kupiga soga kumuhusu huyu mheshimiwa sana.
Mimi nilishaacha kupeleka nguo zangu pale Alpha Dry Cleaners toka nilipogundua kwamba namfaidisha fisadi huyu ili aendelee kutuibia watanzania. Lakini huyu Kitilya pale TRA amechanjia au ni kwa baba yake. Haya yote yanatokea chini yake na kwa kweli kama Chechetuka alivyosema yeye na mtoto wa huyo mwizi wetu ni chanda na pete!
Heshima kwako mkuu. Lakini sauti za wanaomlilia Mungu hazipotei bure. Iko siku Mungu atawatia ujasiri wale wenye mamlaka na kuwatendea haki watu hawa!
samahani naomba kujua kama manywele entertainment ni yake pia.
haya sasa mwashudia wenyewe huyu ndiye anayetaka kushika nchii hii yangu macho mtoto wake ana biashara nyingi sana za utapeli wa kuwaibia watanzania wako na kaofisi kao kengine pale maeneo ya ubalozi wa marekani ukifika pale kazi zao azijulikani ni magari ya kifahali na mtoto wa lowasa muda mwingi anakuwa pale na mkwe wake lowasa pia wanakuwepo ni muda wote unakuta wako bize yan kweli hawa watu wanatupeleka pabaya sana jaman lowasa huyu iko siku yake
Hebu mpe heshima yake bwana! Yaani yeye aingie biashara ya kuuza kucha za bandia na wigs ndo ifanywe na mkubwa huyu? Ile ni ya mabinti wa mjini hapa!
Mzee! huyu udobi wake siyo kama ule wa wazee wa kule mjini wenye kameza na pasi ya mkaa. Mwenzio kawekeza kweli kweli na nasikia analazimisha mahoteli kupeleka mashuka na mataulo kwake vinginevyo kodi wanapandishiwa na kutishiwa kulipuliwa kwamba hawalipi kodi. Jamaa amekuwa akimchochea boss wa TRA kuwa-black mail wafanyabiashara ili hatimaye wamuunge mkono au vinginevyo biashara zao zipigwe kufuli na kupewa mizigo ya kodi bandia. Iko kampuni moja ya wanafamilia wawili ambao sasa wamelazimika kuunga mkono harakati zake za urais ili kunusuru biashaa zao.
Mzee! huyu udobi wake siyo kama ule wa wazee wa kule mjini wenye kameza na pasi ya mkaa. Mwenzio kawekeza kweli kweli na nasikia analazimisha mahoteli kupeleka mashuka na mataulo kwake vinginevyo kodi wanapandishiwa na kutishiwa kulipuliwa kwamba hawalipi kodi. Jamaa amekuwa akimchochea boss wa TRA kuwa-black mail wafanyabiashara ili hatimaye wamuunge mkono au vinginevyo biashara zao zipigwe kufuli na kupewa mizigo ya kodi bandia. Iko kampuni moja ya wanafamilia wawili ambao sasa wamelazimika kuunga mkono harakati zake za urais ili kunusuru biashaa zao.
Haya, tusubiri response ya TRA
Fagio la chuma latakiwa lianzie kumwondoa mheshimiwa mstaafu na lishuke chini kwa hawa vibaraka wake walio kwenye taasisi mbalimbali nchini.
vinginevyo kila siku yatakuwa yanaibuka mapya tena yatakuja mazito zaidi kwa sababu ana vimba kichwa kwa kutokuchukuliwa hatua zozote
Hapa umenena mkuu. Jamaa ana jeuri ya ajabu na kama ulivyosema ataanza kuiba hata vyungu vya maua pale ikulu
Jee mukifanya mgomo wa business zake kama hizo za dry cleaning hazitasaidia?