Kampuni za Bima zinasaidia au magumashi? Umewahi kufidiwa pesa, kutengenezewa au kubadilishiwa gari baada ya ajali

Kampuni za Bima zinasaidia au magumashi? Umewahi kufidiwa pesa, kutengenezewa au kubadilishiwa gari baada ya ajali

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Kampuni za Bima hujinadi kumsaidia muhanga pale mali zake zinapopatwa na uharibifu kumfidia aidha kwa kumpa pesa, kumrekebishia au kumbadilishia mali nyingine.

Je, mali yako uliyoikatia bima ilipoharibika walikusaidia kweli au ni uswahili?

Kwenye fidia
  • Matengenezo yalikuwa ya kiwango kinachoridhisha?
  • Fidia ya pesa iliendana na thamani ya mali?
  • Mali iliyobadilishwa ina ubora kama mali ya mwanzo?
 
Zanzibar insurance comprehesive walininunulia gari nyingine mpya.

NHIF wameshakuwa waswahili, inshort inategemea unataka bima ya nini choose wisely.
Baada ya muda gani, mlipitia michakato ipi, connections / Rushwa ?
 
Me nimeona kwa jamaa yangu, uwa siombei initokee mimi.

Gari iliungua moto akapewa hela. Ila kuna % zinakatwa kutoka kwenye ile thamani yake.

Mfano ulithaminisha gari lako Mil 10 siku ya kutakiwa kupewa hela (kama lipo totaled kabisa) nadhani unapewa like 75-85%

PS: tunaongelea bima ya matajiri comprehensive sio timiza wajibu 3rd party.
 
Strategis walilipa duka lililobadilisha hichi kioo full price no questions asked.
IMG-20231218-WA0002.jpg

Comprehensive inasaidia
 
UAP walinifidia Discovery 4 yangu iliyoungua ila walikata 25% mbwa wale
 
Aisee kumbe hizi comprehensive inategemea kampuni na kampuni.
Total loss wengi wanalipa, ila ukidanganya dhamani ya mali yako ndio kimbembe.

Gari ya 70M Kama uli declare 40M utalipwa hiyo 😀
 
Zanzibar insurance comprehesive walininunulia gari nyingine mpya.

NHIF wameshakuwa waswahili, inshort inategemea unataka bima ya nini choose wisely.
Walikununulia Gari mpya au walikupa fedha ili ukanunue Gari jingine?
 
3rd party janga lolote lile imekula kwa tyuu
Hapana, inacover kwa yule ambaye umemsababishia ajari, kama wewe huna koda aliyesabisha ajari issurance yake ndio inacover damage kwako.
 
Usiruhusu uzoefu wa watu wengine ukupe hofu ya kukata bima kubwa. Muhimu ni kufuata mwongozo sahihi. Zingatia mambo haya:

1. Kampuni ya Bima: Chagua kampuni yenye rekodi nzuri ya huduma bora.
2. Thamani Halisi ya Gari: Hakikisha unaweka thamani halisi ya gari lako kwenye mkataba wa bima.
3. Umiliki Sahihi: Mmiliki halali wa gari anatakiwa kutambulika kwenye mkataba wa bima.
4. Kuchangia Madai: Fahamu asilimia ya mchango wako kwenye madai (excess)
5. Kiasi cha Madai: Tambua kiwango cha chini unachoweza kudai kutoka kwa kampuni ya bima.
6. Uwasilishaji wa Nyaraka: Wasilisha nyaraka zote muhimu kwa wakati pindi unapowasilisha madai.
Kwa msaada zaidi kuhusu bima na madai, wasiliana nami kwa 0765827355.
 
Back
Top Bottom