DOKEZO Kampuni za kukusanya Taka mitaani zizingatie suala la afya kwa wafanyakazi wake

DOKEZO Kampuni za kukusanya Taka mitaani zizingatie suala la afya kwa wafanyakazi wake

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Ni mara nyingi nimeona haya magari ya wanaokusanya taka mitaani, na wale wanaopitia taka majumbani wakifanya kazi zao katika mazingira hatarishi yasiyojali afya ya ya watu wale.

Wamekuwa wakizoa taka au kupakia taka kwenye magari huku hawana vifaa vya kuwasaidia angalau kupunguza kama sio kujikinga kabisa na madhira ya kazi hasa ukizingatia kazi yao inahusisha taka na taka ni sehemu ambayo ni rahisi mtu kupata magonjwa.

Wanakiwa hawajavaa viatu maalumu wala mipira migumu mikononi achilia mbali kukosa vitu vya kuwazuia kuvuta harufu kali ya uchafu muda wote wawapo ndano ya gari la taka na pia wanapokusanya na kuzipandisha humo.

Wanakuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, kuhara na kuhara damu na aina nyingi nyingi za magonjwa kwani wanaogelewa kwenyw lindi la taka ambazo zimeshaona na kuweka wadudu

Mamlaka inabidi zifanye juhudi za makusudi kuwalazimisha wenye kampuni na wafanyakazi husika kuchykua tahadhari dhidi ya afya zao kwani ni rahisi kusambaza magonjwa motaano iwapo watayapata maana wanaishi uraiani.

 
Hoja yako ni ya MSINGI sana kiongozi,ukiongea na wamiliki wanasema jamaa ni WAKAIDI,sijui ni kujikatia tamaa na maisha?

Nadhani mamlaka za kusimamia afya za wafanyakazi,ngazi ya Halmashauri hawana budi kuingilia kati
 
Back
Top Bottom