Kampuni za mabati za kuziogopa

Kwa sisi wavunja ukuni bei Ya ya ALAF kuimudu ni kazi sana,Nilimunua Bati bomba ila hazikukaa muda zikapauka sanaa so karibu kampuni ingine sio bati bomba mzee.
 
Safi sana mkuu.Mimi mwenyewe nipo najikusanya Mdogo Mdogo nije niezekee bati za ALAF,naona hata muda wa guarantee kwao ni mrefu sana tofauti na hao wengine.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Sasa Hapo Utapigwa Nunua Bati Za Kawaida Tu
 
Kuna jambo wengi mnakosea sana. Kuna rangi zinapauka haraka sana haijalishi umenunua wapi na ndio maana kuna kampuni hazizalishi hizo rangi rangi za damu a mzee na blue (blue bahari) hata ungenunua wapi zinapauka haraka.

Hizo rangi nyingine zote after 5yrs zitaanza pauka soma disclamer za makampuni yote utapata majibu.

Mwisho ubora wa bati hupimwa kwenye grade G26, G28, G30 na sio rangi. Hivyo kama wameptishwa na TBS basi grades husika hazina shida.

Upigaji wa bati na aina ya misumari tafanya bati idumu muda gani. Kwa mikoa ya pwani lazima utumie misumari yenye mpira na lazima ilibane bati kutokuruhusu hewa/unyevu pale ulipotoboa kwani kuoza kutaanzia hapo na baada ya miaka michache kutavuja.


Nunua bati rangi grey, brick red, dark green piga kwa kufuata utaratiu na misumari husika utanishukuru
 
Alaf sqm moja 22000-23000 wakati kwa hao wachina 17000-18000 tofaut kubwa sanaa
Kama Bati ni gharama kuna Makuti jamani.

Pigania kitu bora sio bora kitu.
Haiingii kichwani kuacha kitu bora kwa tofauti ya buku 5 au 6.
 
Hapo kwenye rangi ya bati kuwa inachangia kupauka kwake sio sawa!! Kwa bati za ALAF, damu ya mzee huu ni mwaka wa 12,bado ipo kwenye ubora wake, walioezekea rangi hiyo ila kamouni ya sunshare baada ya miaka 2 tu sasa imeshapauka sana, sijui ikifika miaka 10,zitakuwa rangi ya sufuria
 
Muhimu niko ndani,mkono wangu ndio ulipofikia,kuliko kukosa kabisa wacha lipauke tu...
 
Nakubalina nawe kwenye brick red, hata bati za makampuni haya ya TSH 23,000 zinachelewa kupauka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…