KERO Kampuni za mawasiliano kwanini mlazimishe mteja kupata huduma ambayo hana haja nayo?

KERO Kampuni za mawasiliano kwanini mlazimishe mteja kupata huduma ambayo hana haja nayo?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Angyelile99

Member
Joined
Oct 9, 2023
Posts
89
Reaction score
164
Hivi kuna haja gani ya kumlamisha mteja kupata huduma ambayo hana haja nayo?. Mtu anahitaji kuunga kifurushi cha data yaani internet bundle, lakini anapewa dakika ama na sms bundle.

Sasa kwanini usiwekwe utaratibu wa uwanja mpana wa machaguzi ya vifurushi ili kumfanya mnunuzi kuwa huru zaidi? Kuna wizi wa kidigitali unaofanyika kwa wananchi. Zile percent za bundle asilolitumia huwa zinaelekea wapi?
 
Tuache ulalamishi,
Zipo bando zenye sms tupu, dakkka tupu n mb tupu,
Fanya uchunguzi vema
 
Hivi kuna haja gani ya kumlamisha mteja kupata huduma ambayo hana haja nayo?. Mtu anahitaji kuunga kifurushi cha data yaani internet bundle, lakini anapewa dakika ama na sms bundle.

Sasa kwanini usiwekwe utaratibu wa uwanja mpana wa machaguzi ya vifurushi ili kumfanya mnunuzi kuwa huru zaidi? Kuna wizi wa kidigitali unaofanyika kwa wananchi. Zile percent za bundle asilolitumia huwa zinaelekea wapi?
Kero kubwa zaidi kutoka kwa Watoa huduma za mitandao ya simu ni Kuunganishwa kwa lazima kwenye huduma usiyoitaka wala hukuiomba na kisha wanakukata pesa kwa lazima. Hii ni Kero kubwa Sana.

Mbaya zaidi sana, wanakupatia na maelekezo ya kuweza kujitoa kutoka kwenye huduma hiyo uliyounganishwa kwa lazima bila ridhaa yako kwamba utume ujumbe wenye neno 'ONDOA' kwenda kwenye namba fulani wanayokutajia, ukituma ujumbe huo wa kujiondoa kisha wanakukata pesa nyingine tena kama gharama ya kutuma ujumbe kwenye namba hiyo.
Yaani ni kero juu ya kero.
 
Back
Top Bottom