DOKEZO Kampuni za ukopeshaji zinazokiuka sheria na kanuni kwanini hazichukuliwi hatua?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Napenda kuwasilisha kero yangu kuhusu kampuni za mikopo ya mtandaoni.

Serikali ilitangaza hatua za kudhibiti na kuchukua hatua dhidi ya kampuni zilizokuwa zikikiuka sheria na haki za wakopaji. Hata hivyo, hadi sasa kampuni nyingi zinaendelea kutoa mikopo na, pindi mkopaji anapochelewa kufanya malipo, hutumia mbinu zilezile zilizokuwa zikilalamikiwa, ikiwemo vitisho, udhalilishaji na uvunjaji wa faragha za wakopaji.

Swali langu ni: Je, mamlaka husika na vyombo vya dola vimeshindwa kusimamia utekelezaji wa sheria dhidi ya kampuni hizi, au kuna hatua zinazoendelea ambazo umma haujapati taarifa zake?

Wananchi wanahitaji ufafanuzi wa kina na hatua madhubuti ili kuhakikisha sheria zinatekelezwa kwa usawa, kampuni zinazokiuka taratibu zinawajibishwa, na haki za watumiaji wa huduma za kifedha zinalindwa.
 
Sasa utasaidiwa vipi taarifa zako za juu Kwa juu, umetuma kama Anonymous lakini Bado umeshindwa tiririka majina ya kampuni, uzalishaji WA Haina gani, vitisho vipi na mambo mengine ya nje utaratibu na sheria za ukooeshaji.... Mwaga Mchele wamiliki wajirejebishe, wahusika wafuatilie, pia wengine wasijue pata changamoto ulizo pata... Acha woga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…